Mbunge Mhandisi Atashasta Nditiye afariki

Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma, Mhandisi Atashasta Nditiye ambaye amewahi kuhudumu kama Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi akishughulikia Mawasiliano amefariki dunia leo Februari 12, 2021, anaripoti Mwandishi Diramakini (Dodoma).

Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa uhai wake.

Hayo yamethibitishwa leo Februari 12, 2021 bungeni jijini Dodoma na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Job Ndugai.

Spika Ndugai ameeleza kuwa Nditiye alipata ajali siku ya Jumatano Februari 10, mwaka huu na alipatiwa matibabu katika Hospitali ya General Dodoma kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ambako alifariki Dunia leo saa 4 asubuhi.

Aidha, kufuatia kifo hicho, Bunge limehairisha shughuli zake kwa leo hadi kesho.Mhandisi Atashasta Justus Nditiye alizaliwa Oktoba 17, 1969 (51) na ni mwanasiasa mahiri aliyeanza kujihusisha na mambo ya kisiasa hapa nchini tangu mwaka 1990 akiwa mwanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hadi leo.

Wakati wa kipindi cha kwanza cha Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli kuanzia mwaka 2015 hadi 2020, Mhandisi Nditiye alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news