MOI kwa kushirikiana na KCMC zaanza kutoa huduma za kupasua ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu

Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa kushirikiana na Hospitali ya rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) zimeanzisha ushirikiano wa kutoa huduma za kibingwa za upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu kwa wakazi wa Kanda ya Kaskazini ili kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kuafuata huduma hizo Dar es Salaam au kwenda nje ya nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface amasema, kuanzishwa kwa huduma za kibingwa za upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu katika hospitali ya KCMC ni azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi na kuwapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma Dar es Salaam.

“Tumekuja hapa kwa ajili ya kuanzisha ushirikiano na wenzetu hawa wa KCMC katika eneo la upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu ili wagonjwa wenye magonjwa hayo wapate huduma hizo hapa pasipo ulazima kuja MOI, wataalamu wetu wamekuja kufanya tathmini ili tuwashauri namna bora ya kutoa huduma na pia kuwajengea uwezo wataalam wa hapa,"amesema Dkt. Boniface
Ushirikiano baina ya MOI na KCMC unatekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi ili kuwapunguzia usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo Dar es Salaam au nje ya nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news