




Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) Dkt. Benjamin Ndimila akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wakala yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mhe. Ndejembi amewaasa watumishi hao kuendelea kuchapa kazi wakati changamoto zao zikifanyiwa kazi.
Wakala ya Ndege za Serikali ilianzishwa tarehe 17 Mei, 2002 kwa mujibu wa Sheria ya Wakala ya Ndege za Serikali Na.3 ya Mwaka 1997 kwa lengo la kuboresha huduma na kuimarisha usalama wa usafiri wa ndege kwa Viongozi Wakuu wa Kitaifa wanaotumia ndege hizo.
Pamoja na jukumu hilo, Wakala ina jukumu la kuratibu kwa niaba ya Serikali ununuzi wa ndege mpya za biashara, kuzikodisha kwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) na kusimamia mikataba ya ukodishwaji wa ndege hizo.