Rais Dkt.Mwinyi asaini kitabu cha maombolezo ya Maalim Seif Sharif Hamad

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisaini kitabu cha maombolezo aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni jijini Zanzibar leo Februari 23,2021.(Picha na Ikulu).

Tukio hilo limefanyika leo Februari 23, 2021 huko katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil, Kikwajuni jijini Zanzibar ambapo Rais Dkt. Mwinyi amesaini kitabu hicho majira ya saa tatu za asubuhi.

Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad alifariki dunia mnano Februari 17, 2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam na kuzikwa huko kijijini kwao Nyali Mtambwe, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kusini Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news