Rais Kenyatta:Ruto kwa tabia hizi unaweza kujiuzulu

Rais wa Jamhuri ya Kenya,Uhuru Kenyatta amemtaka Makamu wake wa Rais, William Ruto kujiuzulu katika nafasi hiyo iwapo anashindwa kujiheshimu kutokana na ukosoaji wake wa mara kwa mara wa Serikali anayoiongoza, anaripoti Mwandishi Diramakini (Nairobi).

Ameyasema hayo leo Februari 12, 2021 wakati akihutubia huko Uthiru huku akihoji kwa nini viongozi wanakuwa ndumila kuwili kuhusu masuala ya kiserikali wakati wenyewe wamo ndani ya Serikali hiyo.

"Kwa kiongozi kuendelea kutumia maneno ya ovyo wakati anahutubia Wakenya...kwa upande mmoja anasema serikali imeshindwa na kwa upande mwingine anasema sisi kama serikali tumefanya maendeleo haya na yale.

"Hii haikubaliki, hauwezi kusema Serikali imeshindwa wakati na wewe unahudumu na wakati huo unaainisha kile ambacho unaoanisha ni mafanikio ya Serikali. Ni vema ukajiuzulu,"amesema Rais.
Uhusiano wa siasa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na makamu wake William Rutokwa muda mrefu umeendelea kudorora baada ya Makamu wa Rais kuonekana kujifanyia mambo yake binafsi kwa kile kinachotajwa kuwa ni kujijenga zaidi ili kuwania nafasi ya Urais uchaguzi ujao nchini Kenya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news