Tanzania mbioni kusaini Mkataba wa Eneo Huru la Biashara ya Utatu COMESA-EAC-SADC

Serikali ya Tanzania imeshiriki katika Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliofanyika kwa njia ya video, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Viongozi wakiendelea kufuatilia mkutano kwa njia ya mtandao.

Katika mkutano huo moja ya ajenda ilikuwa nchi Wanachama kutoa taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa katika kusaini na kuridhia mkataba wa kuanzishwa kwa Eneo Huru la Biashara ya Utatu ya COMESA-EAC-SADC.

Katika mkutano huo Tanzania kupitia Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho imeeleza kuwa ipo katika hatua za kusaini na kuridhia mkataba huo.

Mkutano huo ulioitishwa kwa dharura pia ulilenga kupitia na kujadili rasimu ya mwongozo wa utatu wa usimamizi na ufuatiliaji wa uvukaji salama wa watu na bidhaa mipakani katika kipindi hiki cha Ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho, Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Geofrey Pinda wakifuatilia Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliokuwa ukiendelea kwa njia ya video.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akifuatilia Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliokuwa ukiendelea kwa njia ya video.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho akichangia jambo katika Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliofanyika kwa njia ya video.
Badhi ya Watumishi wa Serikali waliohudhuria Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliokuwa ukiendelea kwa njia ya video wakifualia mjadala uliokuwa ukiendelea.
Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho, Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Geofrey Pinda wakifuatilia Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliokuwa ukiendelea kwa njia ya video.

Jumuiya za COMESA, EAC na SADC baada ya kugundua kuwa nchi mbalimbali ziliaandaa miongozo ya kudhibiti maambukizi ya UVIKO-19 bila kuathiri uchumi na biashara iliamua kuratibu maandalizi ya miongozo ya kikanda ili kuondokana na changamoto za biashara baina ya nchi wanachama. Nchi wanachama zimekubaliana kuwa mkutano uitishwe tena baada ya wiki mbili ili kujadili agaenda hii na kufikia maamuzi ya pamoja.

Katika mkutano huo kwa upande wa Tanzania ulihudhuriwa na Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Geofrey Pinda Watendaji na Maafisa mbalimbali wa Serikali

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news