Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema katika kipindi cha muhula wa pili wa miaka mitano ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli itajikita zaidi katika diplomasia ya uchumi, kuimarisha sekta binafsi, kukuza biashara pamoja na mahusiano na Mataifa mengine duniani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Msimamo wa Tanzania umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi Jijini Dar es Salaam
wakati wa mkutano wake na Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao hapa
Tanzania pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na kuongeza kuwa ni
dhamira ya Tanzania kuhakikisha kuwa ina uwezo wa kukuza biashara na
kuuza bidhaa katika nchi mbalimbali duniani.
“Katika mwaka huu
unaoanza sasa na miaka ijayo katika mhula wa pili awamu ya tano ni
wakati muafaka wa Tanzania kuimarisha diplomasia ya uchumi na uhusiano
mwema baina yake na nchi mbalimbali kwa kuwakaribisha wawekezaji kutoka
nchi hizo katika maeneno ya uzalishaji, viwanda na kuongeza biashara kwa
manufaa ya mataifa yote,” Amesema Prof. Kabudi
Pamoja na mambo
mengine, Prof. Kabudi amewaambia Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya
Kimataifa hapa Nchini kuwa hali ya kisiasa na amani Zanzibar na Tanzania
kwa ujumla imeimarika kuliko wakati wowote hususani mara baada ya
uchaguzi mkuu uliomalizika Octoba, 2020 na kwamba uwepo wa Serikali ya
Umoja wa Kitaifa Zanzibar unachochea kuongezeka kwa uwekezaji na
ufanyaji wa biashara kwa lengo la kukuza uchumi.
Kwa upande
wake Kiongozi wa Mabalozi Dkt. Ahmada El Badasui ambaye pia ni Balozi wa
Comoro hapa nchini ameshukuru kwa uwepo wa mkutano huo ambao unawapa
fursa mabalozi kufahamu masuala mbalimbali yanayoendelea hapa nchini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe William Tate Ole Nasha (Mb) akiongea na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiongea na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
“Nakupongeza
Mhe. Waziri na uongozi wa Wizara kwa kuandaa mkutano huu ambao unatupa
fursa sisi mabalozi kujadili na kujua mambo mbalimbali yanayoendelea
hapa nchini, mikutano kama hii ni muhimu sana kwetu kwani inatusaidia na
kutuwezesha kuboresha mahusiano yetu ya kidiplomasia,” Amesema Dkt. El
Badasui
Balozi wa Comoro hapa nchini na kiongozi wa Mabalozi Dkt. Ahmada El Badasui akitoa neno la shukrani kwa viongozi wakuu wa Wizara (hawapo pichani) kabla ya kumalizika kwa mkutano.
Sehemu ya Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wakifuatilia mkutano.
Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Manfredo Fanti akichangia jambo wakati wa Mkutano. Kulia kwake ni Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba.
Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Manfredo
Fanti ameipongeza Tanzania kwa kuingia uchumi wa kati na kwamba Umoja wa
Ulaya uko tayari kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha Uchumi wa
Tanzania unaendelea kukua na kuimarika.
Mkutano huo wa Mabalozi
na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa umehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe William Tate Ole
Nasha, Katibu Mkuu Balozi, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge na
Wakurugenzi na Wakuu wa Idara na vitengo vya Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Tags
Kimataifa