Makamu Mwenyekiti wa Wanajangwani, Yanga SC, Fredrick Mwakalebela amesema kwa sasa timu yao haitendewi haki na mamlaka zote zinazosimamia soka hapa nchini likiwemo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kamati ya Waamuzi pamoja na Kamati ya saa 72, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Ameyasema hayo Februari 19, 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Jiji la kibiashara nchini Tanzania la Dar es Salaam.
Amesema, katika mchezo wao na Mbeya City walinyimwa penati mbili za wazi ambazo walistaili kuzipata na zingepelekea wao kushinda mchezo huo na sio kupata alama moja tu.
"Kama kuna bingwa kaandaliwa basi apewe kombe tujue moja, tunatarajia kamati husika zitatoa maamuzi katika hizo mechi zetu mbili na hao waamuzi wachukuliwe hatua stahiki tusitolewe kwenye mstari wetu wa kutwaa ubingwa msimu huu.
Pia amesema, mbali na mchezo huo hata mchezo na Kagera nao walinyimwa penati ambazo zingewafanya kupata alama tatu badala ya kupata moja, huku akikiri kuamini mamlaka hizo kuna timu inayoandaliwa kuwa bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
"Tumewakosea nini mpaka mnatufanyia hivi, au hatustahili kucheza Ligi ya Tanzania tujue, hivi vitu vinavyofanyika uwanjani vinawafanya hata mashabiki kukosa uvumulivu na kufanya fujo, Yanga tumechoka kuonewa waziwazi,"amedai.
Hayo yanajiri ikiwa Yanga SC imetoka sare ya bao 1-1 na Mbeya City mchezo uliopigwa jijini Mbeya ikiwemo sare nyingine dhidi ya Kagera Sugar ya bao 3-3 kwenye Uwanja wa Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo, Mwakalebela amesema wanatoa siku 14 kwa Afisa Habari wa Simba SC, Haji Manara kuhakikisha anaomba radhi hadharani kutokana na kauli zake ambazo amedai zimekuwa zikidhalilisha chapa yao ambayo wametumia muda mrefu kuijenga.
''Kuna mtu anaitwa Haji Manara, amekuwa akidhihaki sana brand yetu mpaka ametuletea matatizo na mdhamini wetu, tumempa siku 14 ajitokeze hadharani kuomba radhi na tumemfikisha kwa TFF pia hatua zichukuliwe na iwe fundisho kwa wengine,"amesema Mwakalebela.
Aidha, Mwakalebela ametoa ufafanuzi kuhusu suala la Bernard Morrison, ambapo ameitaka TFF kuchukua hatua. ''Suala la Morrison tumeshapeleka malalamiko yetu kwa TFF kuwa kuna mkataba feki tunaomba tuitwe kuthibitisha lakini hatujaitwa, ila la mtu wetu Hassan Bumbuli limefanyiwa kazi na akafungiwa, kiukweli tunashangaa,''amesema.

Tags
Michezo