Mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Kagera, Geita, Mara, Mwanza, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Kigoma, Tabora, Katavi, Dodoma, Singida, Ruvuma, pamoja na Kusini mwa mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
..........
Mikoa ya Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Lindi na Mtwara: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo
machache na vipindi vya jua.
...........
Mikoa ya Dar es Salaam na Tanga, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na (Visiwa vya Unguja na Pemba): Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
..........
VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango cha chini
cha joto cha joto
ARUSHA 28°C 18°C
D'SALAAM 32°C 25°C
DODOMA 29°C 18°C
KIGOMA 29°C 22°C
MBEYA 26°C 18°C
IRINGA 24°C 17°C
NJOMBE 23°C 13°C
MWANZA 28°C 20°C
TABORA 27°C 20°C
TANGA 32°C 24°C
ZANZIBAR 32°C 26°C
...........
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 40 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa.
Matarajio kwa siku ya Jumanne tarehe 16/02/2021: Kupungua kwa mvua katika maeneo mengi ya nchi.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 14/02/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.