Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today February 20th, 2021
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO:
TAREHE: 20/02/2021.
Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Mbeya na Songwe: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua.
..........
Mikoa ya Lindi na Mtwara: Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
........
Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Tabora, Iringa, Njombe, Dar es salaam, Tanga, Pwani ( ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Visiwa vya Unguja na Pemba: Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.........
Mikoa ya Manyara, Kilimanjaro, Arusha Dodoma, Singida, Ruvuma na Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
..........
VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango chachini
cha joto cha joto
ARUSHA 27°C 15°C
D'SALAAM 31°C 25°C
DODOMA 30°C 20°C
KIGOMA 26°C 21°C
MBEYA 27°C 16°C
IRINGA 28°C 17°C
NJOMBE 21°C 13°C
MWANZA 26°C 22°C
TABORA 28°C 19°C
TANGA 32°C 24°C
ZANZIBAR 31°C 24°C
..........
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini; na kwa kasi ya km20 kwa saa kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Madogo hadi makubwa kiasi.
Matarajio kwa siku ya Jumatatu tarehe 22/02/2021: Kuongezeka kwa mvua.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 20/02/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
MATARAJIO YA HALI MBAYA YA HEWA KWA SIKU TANO ZIJAZO.
..........
Jumamosi 20-02-2021
HAKUNA TAHADHARI
..........
Jumapili 21-02-2021
HAKUNA TAHADHARI
.........
Jumatatu 22-02-2021
ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa
baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha,Kilimanjaro, Manyara, Dar es Salaam,Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia),Kaskazini mwa Morogoro, Lindi na Mtwara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI
Athari zinazoweza kujitokeza: Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji.
Tafadhali zingatia na ujiandae.
...........
Jumanne 23-02-2021
ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa
baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha,Kilimanjaro, Manyara, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Morogoro, Ruvuma, Lindi na Mtwara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA:WASTANI
Athari zinazoweza kujitokeza: Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji.