UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO:
TAREHE: 22/02/2021.
Mkoa wa Ruvuma, Mbeya, Songwe, Iringa, Rukwa, Njombe, Manyara, Kilimanjaro, Arusha pamoja na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
..........
Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Kigoma, Tabora, Katavi, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Dar es Salaam,Singida, Dodoma, Lindi, Mtwara, Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba: Inatarajiwa kuwa na
Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
...........
ANGALIZO
VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA ARUSHA, KILIMANJARO NA
MANYARA.
VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango cha chini
cha joto cha joto
ARUSHA 25°C 17°C
D'SALAAM 31°C 25°C
DODOMA 29°C 19°C
KIGOMA 29°C 20°C
MBEYA 29°C 16°C
IRINGA 27°C 17°C
NJOMBE 21°C 12°C
MWANZA 26°C 22°C
TABORA 27°C 18°C
TANGA 32°C 25°C
ZANZIBAR 32°C 25°C
.........
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 20 kwa saa kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani yote.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Madogo.
Matarajio kwa siku ya Jumatano tarehe 24/02/2021:
Mabadiliko Kidogo.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 22/02/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
Jumatatu: Tarehe 22-02-2021
ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI
ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: MDOGO
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: KIKUBWA.
Athari zinazoweza kujitokeza: Makazi kuzungukwa na maji pamoja na kucheleweshwa kwa shughuli za usafirishaji.
Tafadhali zingatia na ujiandae.
...........
Jumanne 23-02-2021
ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI
Athari zinazoweza kujitokeza: Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na kucheleweshwa kwa shughuli za usafirishaji.
Tafadhali zingatia na ujiandae.
...........
Jumatano 24-02-2021
HAKUNA TAHADHARI
Alhamisi 25-02-2021
HAKUNA TAHADHARI
Ijumaa 26-02-2021
HAKUNA TAHADHARI