Mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Tabora, Katavi, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Mbeya, Songwe, Iringa, Rukwa, Njombe, Dodoma na Singida inatarajiwa Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.........
Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu inatarajiwa Hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.........
Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Visiwa vya Unguja na Pemba, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro inatarajiwa Hali ya mawingu kiasi, Mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
........
Mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na Arusha inatarajiwa Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
...........
KIWANGO CHA JUU CHA JOTO HAPA NCHINI: Ni nyuzi joto 33 (33°C) katika maeneo ya Dar es salaam, Tanga na Zanzibar
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kwa kasi ya km 20 kwa saa kutoka Kaskazini Magharibi kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Madogo hadi Makubwa kiasi.
Matarajio kwa siku ya Jumanne tarehe 02/03/2021: Mabadiliko Kidogo.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 28/02/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.