ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (pamoja na kisiwa cha Mafia),Tanga, Kaskazini mwa mikoa ya Morogoro na Lindi, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI
Athari zinazoweza kujitokeza
Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji.
JUMATANO: 10/02/2021
ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya
mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (pamoja na visiwa cha Mafia), Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Rukwa, Njombe, Iringa, Dodoma, Singida na Manyara.
UWEZEKANO WA KUTOKEA:WASTANI
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI
Athari zinazoweza kujitokeza Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji.
ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2, limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa
vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.
Athari zinazoweza kujitokeza Kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi
........
ALHAMISI: 11/02/2021 HADI JUMAMOSI : 13/02/2021
HAKUNA ANGALIZO
Imetolewa leo 09/02/2021
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA