Vikundi 21 vyanufaika na mikopo ya asilimia 10 Manispaa ya Kigoma

Jumla ya vikundi 21 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wamenufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kutoka katika mapato ya ndani ya halmashauri,anaripoti Fred Elisha (Kigoma).
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mwailwa Pangani amesema kati ya vikundi hivyo, viwili ni vya walemavu, saba ni vijana na 12 ni vya wanawake ambavyo jumla vilikopeshwa kiasi cha sh. 80,277,500.

Pangani amefafanua kuwa halmashauri yake ilivikopesha fedha vikundi vya wanawake kiasi cha sh. 53,500,000, vijana sh 24,500,000 na walemavu sh 2,277,500 fedha ambazo walizitumia kufanyia biashara na ujasiriamali.
Miongoni mwa vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo katika Manispaa ya Kigoma ni Kikundi cha Watu wenye ulemavu cha Nyota Njema hujishughulisha na utengenezaji wa Sabuni,Ushonaji wa Mashuka na biashara ya usafirishaji wa abiria kwa njia ya bajaji.

Katibu wa Kikundi hicho aliyejitambulisha kwa jina la Akizimana amekiri kikundi chao kupokea mkopo wa sh 5,000,000 kutoka Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo kikundi kimekwisharejesha kiasi hicho na wanajiandaa kuomba mkopo mwingine wa sh.milioni 13.

Naye Aisha Kigwiza, Mwenyekiti wa Kikundi Cha Tegemeo kinachohusika na uzalishaji na utengenezaji çhaki eneo la Ujiji amesema kikundi chao chenye wanachama kilipokea sh.5,000,000 za mapato ya ndani ya halmashauri na kimekwisharejesha fedha zote na kinajiandaa kuomba mkopo mwingine ili kiweze kupanua shughuli zake mjini humo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha Aquaculture Experty kinachojishughulisha na ufugaji wa samaki, uuzaji wa Vyakula na vinywaji katika mgahawa uliopo katika Mwalo wa Kibirizi Mashaka Matiko Pamoja na kukiri kupokea fedha kiasi cha sh 5,000,000 kutoka katka mapato ya ndani ya halmashauri aliipongeza serikali kwa hatua hiyo ya kuwapa vijana mikopo isiyo na riba

"Kwa kweli naipongeza Serikali na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kuwa sasa sisi vijana wa kikundi hiki hatuna hofu ya kutoajiriwa kwani kupitia shughuli zetu tumeweza kujiajiri na kuwaajiri baadhi ya vijana wenzetu walipo mtaani na hawana kazi,” amesema.

Katika mwaka wa fedha 2020/2021 Manispaa ya Kigoma Ujiji imetenga kiasi sh 77,645,546 na tayari halmashauri yake imekwishakopesha sh 21,500,000 sawa na asilimia 27 hadi februari, 2021 kiasi cha Million 40 kitakopeshwa kwa vikundi vingine baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu kutoka kwa wataalamu wa Maendeleo ya Jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news