Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) imewataka wajasiriamali wadogo kuwa na utamaduni wa kupima bidhaa zao jambo ambalo litawasadia kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za kibiashara na kiuchumi.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (katikati) akikata utepe kuzindua Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonyesho ya bidhaa yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizingumza leo Februari 28, 2021 jijini Dar es Salaam katika Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonyesho ya bidhaa, Meneja wa Mawasiliano Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), Bi. Irene John, amesema kuwa lengo la kushiriki maonyesho hayo ni kutoa elimu kwa wajasilimali wadogo ili waweze kupiga hatua katika soko la ushindani.
Bi. John amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu ili wajasiliamali wafungashe bidhaa zao kwa kuzingatia vipimo sahihi jambo ambalo litawasaidia kufanya biashara kwa ufanisi mkubwa.
“Tumefika katika uchumi wa kati, mjasiliamali mdogo hawezi kufikia uchumi wa kati kama hatumii vipimo sahihi,”amesema Bi. John.
Ameeleza kuwa, wana jukumu la kuendelea kuwaelimisha wajasilimali wadogo na jamii kuwa ujumla ili waweze kuwa na uelewa mpana katika kuhakikisha wanazalisha bidhaa bora.
Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), Bi. Grory Mtana, amesema kuwa wapo katika maonyesho hayo kwa ajili ya kuwasaidia wajasilimali wadogo ili waweze kuingia katika masoko ya kimataifa.
“Tunawaelimisha namna bora ya kufungasha bidhaa zao kwa kutumia vipimo sahihi ili waweze kufanikiwa na kufika masoko ya mbali,” amesema Bi. Mtana.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea katika banda la Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) katika Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonyesho ya bidhaa yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Tehama Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Bi. Rehema Michael, ametoa wito kwa wajasiliamali kushiriki katika maonyesho hayo ili waweze kupata ushauri ambao utawasaidia kufungasha bidhaa vizuri na kukizi masoko ya ndani na nje ya nchi.
Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonyesho ya bidhaa yamefunguliwa rasmi leo Februari 27 mwaka huu na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe.
Kutoka kushoto ni Meneja wa Mawasiliano Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), Bi. Irene John, Afisa Vipimo WMA Bi. Grory Mtana, Afisa Tehama WMA Bi. Rehema Michael, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu WMA, Bi. Stella Kahwa wakimsilikiza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (wa kwanza kulia) wakati alipotembelea banda la WMA
Maonyesho hayo yanafanyika kwa muda wa siku saba katika viwanja vya Posta /TTCL Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Tags
Uchumi