Waziri wa zamani wa Katiba na Sheria, Balozi Bakari Mwapachu amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.
Andrew Nkuzi ambaye ni msemaji wa familia ya Mwapachu ameieleza Mwananchi Digital kuwa mwili wa mbunge huyo wa zamani utawasili Tanga leo jioni na utahifadhiwa nyumbani kwake Mchukuuni kata ya Tangasisi.
Amesema mazishi ya kiongozi huyo yatafanyika kesho Jumamosi Februari 13, 2021 kijiji cha Pande Wilaya ya Tanga.
Mwapachu alikuwa Mbunge wa Tanga kuanzia mwaka 2000 hadi 2010 alipomwachia kijiti Omar Nundu (marehemu) na amewahi kushika nafasi za mbalimbali za uongozi serikalini katika vipindi tofauti.

Tags
Habari