Muziki wa kizazi kipya umeendelea kukua kwa kasi kubwa hapa nchini na Duniani kwa ujumla, hali ambayo imesababisha vijana wengi kuvutiwa na kuhamasika kufanya muziki huo kwa ubora wa hali ya juu, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.
Tofauti na miaka ya nyuma vijana wengi walikuwa hawajishughulishi na muziki kutokana na sababau mbalimbali, lakini kubwa ikiwa kukosa sapoti toka maeneo mbalimbali mfano serikali na jamii.
Muziki ni kifaa muhimu kinacholeta mabadiliko katika jamii, muziki unaweza ukawafikia mamilioni ya watu na kwa kuhamasisha jamii kuhusu changamoto za kijamii, kiuchumi na kimazingira ambayo ndio msingi wa maendeleo endelevu SDGs.
Aidha, Muziki unaendelea kuwa chanzo cha ajira na uchumi lakini muziki wenyewe hauwezi kuwa kifaa muhimu bila ya mchango wa mwanadamu
Katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli kupitia Wizara husika ya Michezo imekuwa ikishirikiana na wasanii na mfano hata wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana tulishuhudia wasanii mbalimbali wakiwemo wanamuziki wakifanya kampeni hivyo inaonyesha wazi kwamba wana mchango mkubwa sana katika kufikia maendeleo.
Kwa hali hiyo ni wazi kwamba sasa serikali imekuwa ikifuatili kazi mbalimbai za wasanii na hivyo kutoa hamasa kwa vijana wa kitanzania kujiingiza kwenye sekta ya muziki lengo kubwa likiwa ni kujikwamua kiuchumi.
Tanzania imekuwa na wasanii wengi vijana ambapo wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika anga la muziki wa kizazi kipya na hatimaye kutambuli ndani na nje ya nchi na kufanya vijana wengi kujiajiri.
Sekta ya muziki ni miongoni mwa sekta ambayo imekuwa ikitoa ajira kwa vijana kwa kujiajili wenyewe hivyo ni jukumu la serikali kuhakikisha sekta hiyo inasimamiwa vizuri ili vijana wavutiwe zaidi kuingia huko.
Ukiachilia mbali wasanii wakubwa na wanaofanya kazi nzuri katika sekta ya muziki unaowafahamu, Kijana mwanamuziki Uwezo Mtenda Khamis (26) a.k.a Ability ni mwanamuziki wa kizazi kipya ambaye kiukweli amekuwa akifanya vizuri na hata kupelekea wasanii wakubwa kuwashirikisha kwenye nyimbo zake.
Katika mahojiano na Mwandishi DIRAMAKINI, akizungumzia safari yake ya muziki,Ability amesema kuwa toka akiwa na umri mdogo alikuwa anapenda sana kuimba na alikuwa akiimba kanisani.
Anasema alianza kujifunza kwa kuimba nyimbo za wanamuziki mbali mbali kama marehemu Msafiri Diof na kwa kipindi hicho alikuwa akimpenda msanii T.I.D na yeye ndipo alipo hamasika kuingia kwenye muziki.
Anasema kutokana na kupenda sana kuwa msaii alilazimika kuacha shule akiwa kidato cha pili na ndipo alipoamua kutoka Mwanza alipokuwa akiishi na wazazi wake na kuja Jijini Dar es salaam.
Anasema mwaka 2018 alirekodi nyimbo yake ya kwanza ijulikanayo kwa jina la 'Bosi Vumbi' ambapo aliitoa rasmi mwaka jana ambapo kabla ya kuutoa rasmi mwaka 2019 alitoa audio na video ya wimbo wa 'Pepeta'.
Anasema pia alitoa kibao kingine cha Marue rue ambacho kilichelewa kutoka kutokanana na sababu mbalimbali, msanii Ability ambaye yupo chini ya kampuni ya Panoramani Entertaiment anasema akiwa chini ya kampuni hiyo tayari amekwisha toa nyimbo mbili ambazo ni Yaishe na Nipe ambazo amefanyia Mombasa nchini Kenya.
Anasema Julai 2020 alitoa nyimbo zingine mbili ya Chochea ambayo amemshirikisha Juma Nature wimbo uliobamba sana na kuingia hadi Trece TV na kupokelewa vizuri nchini Burundi na Rwanda.
"Chochea bado ipo kwenye playlist ya bongo fleva na inafanya vizuri,ambapo pia wimbo wa Tamu umepokelewa vizuri nao pia umeingia kwenye spotify playlist ya nyimbo 50 bora na zinazotamba sana kwenye mitandao ya jamii hapa nchini.
Anasema kuwa pamoja na mafanikio hayo machache aliyoyapata kutokana na kutambulika kwa nyimbo zake lakini bado anahitaji sapoti kubwa ili aweze kutimiza ndoto zake za kuwa mwanamuziki mkubwa Tanzania na Duniani kwa ujumla.
Anasema hata hivyo bado mambo mazuri yanakuja na muda si mrefu ataachia bonge la collabo
ambalo amemshirikisha msanii mkubwa sana na kuwataka mashabiki ku-follow na ku-subscriber kwenye akauti zake za mitandao ya kijamii ili waweze kufahamu kazi zake.
"Nashukuru kwa sapoti kubwa hadi hapa nilipofikia na nawaomba wasichoke waendelee kutoa sapoti na kushare, ku-request kwa upande wa TV na radio kazi zangu kwenye akauti zangu ambazo kwa upande wa You Tube na Face book ni Saint ability na Insta ni saint_ability.
Ability anataja kampuni alizopitia ukiachilia mbali Panoramani kuwa ni pamoja na Mtaa kwa mtaa na Kusi Star seach Konde Gang.
CHANGAMOTO
Anasema katika safari yoyote ile ya kuelekea mafanikio na kutimiza ndoto ni lazma akumbane na chagamoto mbali mbali ambapo kwa upande wake
amekutana na chagamoto kadha wa kadha kama kutokuwa na kipato cha kutosheleza ambapo inamuia vigumu kusambaza muziki.
Malengo
Anasema ana lengo la kuwa mwanamuziki mkubwa sana Duniani naTanzania kwa ujumla ili aweze kuisaidia nchi yake na jamii ya watanzania yenye uhitaji.kwaujumla .
USHAURI KWA SERIKALI
Mbali na kutoa ushauri kwa serikali Ability amempongeza Rais Magufuli kutokana na serikali anayoiongoza ikiwa mstari wa mbele kuhakikisha sekta ya muziki inakua na vijana wengi ambao wata jiajiri na kupata kile wanachostahili kwa kwamba katika kipindi hiki sasa mambo ya muziki yanakwenda vizuri.
Anaiomba serikali kuwaangalia na kuekeleza macho yao kwa wasanii chipukizi kwa kuwa wanachangamoto nyingi tofati na wasanii wa kubwa.
Pia amewataka watanzania hususani wapenzi wa muziki wa kizazi kipya waweze kusikiliza na kuangalia nyimbo zake kupitia mitandao ya kijamii kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamempa sapoti ya kutosha.
WASANII WAKUBWA
Anawaomba wasanii wakubwa kutengeneza njia ili wasanii chipukizi waweze kupita na pia wasanii wakubwa wasaini mikataba na wasanii chipukizi wapate fursa ya kupenya na kuwa na lebo.
Ability ana viomba vyombo vya habari hususani radio pamoja televisheni kumsapoti kwa kupiga nyimbo zake mara kwa mara ili aweze kutambulika.
Ametaja wanamziki anaowahusudu kuwa ni pamoja na Harmonaise, Dimond ,Ali Kiba na wanamuziki wote wanaofanya vizuri ndani na nje ya nchi.