Kijana Anuary Jabir ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mwezi Februari, 2021 huku Kocha wa Ihefu SC, Zubery Katwila akishinda tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu kwa mwezi huo, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.
Katika hatua nyingine John Nzwalla ambaye ni Meneja wa Uwanja Nelson Mandela uliopo Sumbawanga mkoani Rukwa ameshinda tuzo ya Meneja Bora wa Uwanja wa mwezi Februari, mwaka huu.
Kwa sasa Anuary Jabir amekuwa gumzo kutokana na kasi yake ya upachikaji mabao katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mabao saba aliyofunga kwenye mechi nne alizocheza kuanzia raundi ya pili ikiwa zote alifunga katika mechi dhidi ya JKT Tanzania, Coastal Union, Polisi Tanzania na Kipigwe FC na kumfanya afikishe idadi hiyo ndani ya mechi nne.
Ukiachana na mabao matatu aliyonayo kwenye Kombe la Shirikisho, Anuary hivi sasa ana mabao manne huku akiweka lengo la kufunga zaidi mabao kwenye mechi zijazo hadi awafikie wanaoongoza kwa ufungaji Ligi Kuu Tanzania Bara.
Tags
Michezo