Imeelezwa kuwa, wajumbe wa Kamati ya Taasisi ya Uwazi na Uhamasishaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) wana wajibu wa kuitangaza TEITI ili kuifanya ijulikane ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, wanaripoti Tito Mselem na Godwin Msabala (Dar es Salaam).
Waziri wa Madini Doto Biteko kulia akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Ludovick Utouh kwenye kikao cha Waziri wa Madini Doto Biteko, kilichofanyika Machi 10, 2021 katika Ukumbi wa Samwel Sita uliopo katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Doto Biteko alipokuwa kwenye kikao kati yake na Wajumbe wa Kamati ya TEITI kilichofanyika Machi 10, 2021 katika Ukumbi wa Samwel Sitta uliopo katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.
Waziri Biteko amesema kuwa, mwenyewajibu wa kuifanya TEITI ijulikane ni TEITI wenyewe ambapo ameitaka taasisi hiyo kujitangaza ili wananchi waweze kujua kazi na majukumu ya Taasisi hiyo.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Waziri Biteko amesema kuwa, TEITI iko nyuma kwa maana ya kujulikana ambapo amesema TEITI inapaswa kuwa maktaba na kimbilio la taasisi nyingine kwa sababu, inatakiwa kuwa na jicho la kuona kitaifa na kimataifa litakaloona na kusaidi maendeleo ya uziduaji nchini hasa katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi asilia.
Aidha, Waziri Biteko, ameitaka Taasisi ya TEITI kuhakikisha inafuatilia ili kujua na kujiridhisha mipango na gharama iliyotengwa na migodi wanapotaka kufunga migodi hiyo.
“Naomba nichukue fursa hii kuisisitiza kamati hii kuhakikisha anafanya ziara za mara kwa mara katika migodi yetu hapa nchini ili mjiridhishe na mjionee mamna shughuli na biashara za madini, mafuta na gesi asilia zinavyofanyika,”alisema Waziri Biteko.
“Nataka niwahakikishie kamati ya TEITI kwamba, sisi kama Wizara ya Madini tukotari kuwapatia kiasi chochote cha fedha mtakazo hitaji lakini lazima mtuletee matokeo,” aliongeza Waziri Biteko.
Pia, Waziri Biteto amemtaka mwenyekiti wa TEITI kuisimamia sekta hiyo ya Uziduaji ili ijulikane na ilete matokeo chanya kwa taifa
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI Ludovick Utouh, amempongeza Waziri Biteko kwa kuonesha nia ya kuisadia Taasisi hiyo, ambapo amesema, taasisi ya TEITI itaendelea kutambua mchango wa Wizara ya Madini katika kuchanginngia maedeleo ya Taasisi hiyo.
Aidha, Utouh, amesema kuwa, Kamati ya TEITI ipo tayari kupoke maagizo na maelekezo ya Waziri Biteko na kuwataka wajumbe wote kuwa wazalendo ili walete maendeleo kwa taifa lao.
Kwa upande wake Makamu Katibu Mtendaji wa TEITI Mariam Mgaya amesema, TEITI itaendelea kuhakikisha kuwa, Serikali inaweka mifumo ya uwazi katika usimamizi wa rasilimali madini, mafuta na gesi asilia ili kuboresha ukusanyaji wa mapato na manufaa yanayotokana na shughuli za utafutaji na uchimbaji wa rasilimali hizo.
Aidha, Mgaya amesema, kwa kiwango kikubwa ripoti za TEITI zinahusisha uwekaji wazi wa taarifa za kampuni kubwa na za kati tu, lakini kwa sasa TEITI imepanga kuweka wazi mapato na taarifa nyingine za wachimbaji wadogo.
Tags
Uchumi