Menejimenti na wafanyakazi wa Kampuni ya Diramakini Business Limited ambao ni wamiliki wa www.diramakini umesikitishwa na kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.
Tunaungana na wote kwa dua na sala ili mpendwa wetu apumzike kwa amani. Mungu amlaze mzee wetu mahali pema.
Ni ombi letu kwa Watanzania, katika kipindi hiki kigumu yatasemwa mengi kwa sababu Taifa letu linazungukwa na maadui wengi wa ndani na nje kuliko watu wema, hivyo tusikubali kugawanywa, tuendelee kudumisha umoja, mshikamano na amani ya Taifa letu.
Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji
Diramakini Business Limited
Machi 18, 2021.
SPIKA AUNGANA NA WATANZANIA
Wakati huo huo, Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai
amesema kuwa kufuatia kifo cha Rais Watanzania wanakazi yakuhakikisha
wanaendeleza yale ambayo Rais Magufuli alikuwa akiyafanya katika kipindi
cha uhai wake.
Akizungumza na waandishi wa
habari Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai alisema kuwa Rais alikua mjenga Nchi
hasa katika swala zima la miundombinu na miradi mikubwa mingi kama
elimu, afya na barabara nakusema kuwa Rais ameacha alama katika kila
nyanja.
"Mh.Rais wetu mpendwa John Magufuli
alikuwa ni mpenda maendeleo na katika uhai wake amegusa katika kila
nyanja hakika kaacha alama nakutuachia majonzi makubwa
watanzania,"amesema Ndugai.
Amesema kuwa kazi
zote alizokuwa akizifanya Rais, hotuba alizozitoa bungeni sambamba na
utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2025 zitasimamiwa
na kutekelezwa kwa kuongozwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu
Hassani.
Aidha, ameagiza Wabunge wote waliokuwa
kuwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo warudi haraka na mpaka
sasa wabunge wote wako njiani kurudi dodoma.
Sambamba
na hayo amesema kuwa Rais alikuwa muhimili wa pili wa Bunge hivyo ni
pigo kwa Bunge na amemuachia kazi kubwa mama samia na viongozi wote na
serikali kwa ujumla huku akitoa pole kwa mama Janeth mke wa marehemu,
familia ya marehemu na watu wa Chato na kwa Watanzania wote.
Tags
Habari