Uongozi wa Diramakini Business Limited ambao ndiyo wamiliki wa tovuti ya www.diramakini.co.tz unapenda kuwajulisha wasomaji wetu kuwa, kwa sasa tumerejea hewani kama kawaida baada ya kujipa SIKU MBILI za maombolezo ya mpendwa wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Tulijipa siku hizo mbili tofauti na zile 21 za Kitaifa ambazo tunaendelea nazo kwa kumpa heshima na maombi ya kipekee mpendwa wetu huyo.
Kifo chake si tu kwamba kilitushtua sisi kama wana tasnia bali tuliishiwa nguvu kabisa ya kufanya kazi yoyote.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba, mchango wa Hayati Dkt.Magufuli na moyo wa uzalendo kwa Taifa la Tanzania ulitupa ari na hamasa ya kufanya kazi kwa bidii sisi kama vijana katika kudumisha uzalendo, umoja na mshikamano.
Ikiwa kanuni yetu ya msingi imejikita kuwa, maslahi ya Taifa la Tanzania ni muhimu kuliko jambo lolote na msimamo huo utaendelea kuwa hivyo hivyo hata baada ya kuondokewa na mpendwa wetu Hayati Dkt.Magufuli.
Uongozi wa Diramakini Business Limited unaendelea kurejea wito wa upendo, amani, mshikamano, kuliombea Taifa letu na kuzidi kuyapa maslahi ya Taifa letu kipaumbele iwe wadogo kwa wakubwa ili kuhakikisha tunaiendea ndoto ya Hayati Dkt. Magufuli ya kulipaisha Taifa letu kwenda katika viwnago vya juu kiuchumi na kuondokana na utegemezi.
Pia tunachukua nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ambaye ameapisha Machi 19, 2021 kuchukua wadhifa huo baada ya kuhudumu kwa muda katika nafasi ya Makamu wa Rais,huyu ni mama shupavu, asiyeyumbishwa na mwenye misimamo thabiti katika kutetea maslahi ya Taifa.
Tunatambua misimamo, bidii, usikivu na unyenyekevu wa Mama yetu Samia unavyokwenda kuongeza nguvu ya kuendeleza pale ambapo ameachilia Hayati Dkt. Magufuli ili kulipeleka Taifa letu mbele zaidi.
Ni maombi yetu kwa kila mmoja katika nafasi yake aliyopo akatimize wajibu wake bila kushurutishwa ili tuweze kulipaisha Taifa letu,Mwenyenzi Mungu awape nguvu na afya njema ili tukalitumikie Taifa letu.
Imetolewa leo Machi 20, 21 na
Mkurugenzi Mtendaji,
Diramakini Business Limited.
Kwa maulizo ya habari au matangazo katika hii blog tuwasiliane; diramakini@gmail.com AU 0719254464, Asante.
Tags
Habari