Fainali za shindano la Miss Utalii Tanzania 2020/2021 ngazi za kanda zinaanza rasmi mwezi Machi, 2021, baada ya fainali za kupata washindi wa mikoa yote bara na visiwani kukamilika, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Mbeya).
Tswira ya G.Town Hotel, hoteli ya kisasa inayotoa huduma bora jijini Mbeya.
Hayo yamesemwa na Geogina Saulo ambaye ni Mkurugenzi wa Mashindano Miss Tourism Tanzania Organisation kupitia taarifa aliyoitoa kwa umma leo Machi 1, 2021.
Saulo amesema, jumla ya warembo miamoja na hamsini na tano,wenye mataji ya ushindi wa kwanza hadi wa tano wa mikoa,watashindana kuwania mataji ya kanda za Miss Utalii kanda za Kaskazini (Arusha,Manyara na Kilimanjaro), Kusini (Lindi,Mtwara na Ruvuma), Mashariki (Dar Es Salaam, Tanga, Morogoro na Pwani), Nyanda za Juu Kusini (Njombe, Iringa, Songwe, Katavi, Rukwa na Mbeya), Ziwa (Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu), Kati (Dodoma,Singida na Tabora),na Zanzibar (Unguja na Pemba). Kanda ya Magharibi (Geita,Kagera na Kigoma) iilisha kamilisha fainali zake.
Amesema, kila mkoa utawakilishwa na mshindi wa kwanza hadi wa tano katika fainali za kanda husika, ambapo washindi wa kwanza hadi wa tano wa kila kanda , watawakilisha kanda husika katika fainali za Taifa zitakazo fanyika mwezi Mei,mwaka huu 2020/2021.
Aidha mshindi wa kwanza hadi wa tano wa fainali za taifa watawakilisha Tanzania katika fainali za Dunia na nyinginezo za kimataifa,ikiwemo za Miss Tourism world 2020/2021,Miss Gold Internatiinal 2020/2021,Model of The World 2020/2021,Miss Tourism University World 2020/2021,Miss Tourism East Africa 2020/2021,Miss Tourism africa 2020/2021,Miss Tourism International 2020/2021 n.k
"Uzinduzi rasmi wa fainali za kanda,utafanyika rasmi jijini Mbeya sambamba na fainali za kanda za Miss Utalii Nyanda za Juu kusini 2020/2021,zitakazo fanyika Mwisho wa Mwezi huu katika ukumbi wa kisasa wa Mbeya Modern Hotel( Dhamira) ambazo zitashirikisha jumla ya warembo thelathini wenye mataji ya ushindi wa kwanza hadi wa tano wa mikoa ya Mbeya,Katavi,Rukwa,Songwe,Njombe na Iringa.
"Katika kufanikisha kufanyika kwa mafanuikio kwa fainali hizo za kanda za Miss Utalii Nyanda za Juu Kusini 2020/2021, makampuni na wadau mbalimbali wa maendeleo na utalii wa mkoani Mbeya ,wameanza kujitokeza kudhamini shindano hilo la fainali za kanda,"amefafanua Saulo.
Wadhamini walio jitokeza ni pamoja na hoteli ya kisasa ya G.Town Hotel na GR City Hotel zilizopo jijini Mbeya. Hoteli hizo zimetoa udhamini wa kambi ya washiriki, sambamba na vingozi wakati wa maandalizi hadi kukamilika kwa fainali hizo.
Wakiwa kambini washiriki wa Miss Utalii Nyanda za Juu kusini 2020/2021, watapanda majukwaani kuwania mataji na tuzo za utangulizi kabla ya fainali kuu ya kanda. Watapanda jukwaani katika ukumbi wa hoteli ya GR.City Hotel kuwania tuzo za Urembo na Mitindo 2020/2021, watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Utalii Vipaji 2020/2021 katika ukumbi wa G.Town Hotel Mbeya, na kabla ya kupanda jukwaani kuwania taji kuu la Miss Utalii Nyanda za Juu kusini 2020/2021, washiriki wata panda jukwaani mkoani Songwe kuwania tuzo za Utalii,Uhifadhi na Uwekezaji 2020/2021.
Wakiwa kambini mkoani Mbeya ,washiriki wote wa fainali za Miss Utalii Nyanda za Juu kusini 2020/2021, wakiambatana na waandishi wa habari za magazeti, majarida, televisheni, mitandao ya kijamii, wapiga picha za matangazo, video na filamu, wata tembelea maeneo yote ya vivutio vya utalii na uwekezaji vilivyopo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini,huku wakipiga picha za Filamu,Video,Minato na Matangazo,vilivyo chini ya TAWA,TANAPA,TFS,NCAA na mamlaka nyinginezo za Umma na binafsi.
Akithibitisha GR.City Hotel kudhamini fainai hizo ,meneja mkuu wa hoteli hiyo Ndugu Abihudi Ndelwa, almesema kuwa wameamua kudhamini shindano hilo kutokana na mchango wake mkubwa katika kukuza na kuendeleza sekta ya utalii nchini,lakini pia wamevutiwa na mafanikio makubwa ya shindano hilo kitaifa na kimataifa ikiwemo kuweza kuleta fainali za dunia za Miss Tourism world 2006 kufanyika tanzania , na kuwa shindano la kwanza Tanzania kushinda taji ya Dunia, lakini pia kushinda mataji ya dunia katika kila shindano la Duniua walilo shiriki kwa miaka sta mfululizo, amesema kuwa udhamini wao unakadiliwa kufikia thamani ya shilingi za kitanzania 42,000,000.
Aidha mkurugenzi wa G.Town Hotel alithibtisha kudhamini shindano hilo kwa udhamini wenye thamani ya shilingi 67,000,000 kwaajili ya kambi na huduma nyinginezo. Amesema kuwa wamavutiwa na shindano hilo kutokana na maudhui yake, ambapo G.Town Hotel wanaamini litasaidia kuitangaza Mbeya kitaifa na kimataifa,lakini pia kuhamasisha utalii wa ndani na uwekezaji.
Taswira ya GR CITY HOTEL, hoteli ya kisasa inayotoa huduma bora jijini Mbeya.