Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, tangu kuchaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 alijipambanua kama mtu wa vitendo, tofauti na watangulizi wake.
Namna yake ya kutekeleza majukumu ikiwemo kutumbua majipu ilimpatia mashabiki wengi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania hususan katika Ukanda wa Afrika Mashariki ambako kampeni ya #WhatWouldMagufuliDo iliibuka na kupata umaarufu kwa kusifia utendaji wake usiokuwa na simile katika mapambano dhidi ya ufisadi na kusimamia miradi ya ujenzi wa miundo mbinu bila kuchoka.
Watanzania walizingatia zaidi mtindo mashuhuri wa uongozi wa Magufuli ambao ulikuwa mfano wa kusifiwa na viongozi wengine Barani Afrika.
Kipenzi cha watu
Wafuasi wake watakosa mikutano yake ya mara kwa mara alipokuwa ziarani katika maeneo mbalimbali ambapo alisimama mara kadhaa vituoni kuzungumza na wananchi.
Ziara hizo ambazo mara nyingi ziliibua udhaifu wa watendaji wa serikali zilitangazwa mubashara katika runinga na kupata umaarufu kwa wananchi wengi kutumia fursa hiyo kuelezea matatizo yao huku yakipatiwa ufumbuzi papo kwa papo. BURIHANI SHUJAA WA WATANZANIA HAYATI DKT.MAGUFULI.
RATIBA YA KUAGA MWILI WA JPM
Machi 20- Mwili kupelekwa Uwanja wa Uhuru kwa taratibu za kuaga
Machi 21- Dar es Salaam
Machi 22- Dodoma
Machi 23- Zanzibar
Machi 24- Mwanza
Machi 25- Familia na wakazi wa Geita
Machi 26- Mazishi mkoani Geita.
Tags
Habari