Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud amekwenda kumjulia hali Mzee Machano Khamis Ali nyumbani kwake Mombasa Wilaya ya Magharibi 'B' Mkoa wa Mjini Magharib Unguja, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Unguja).
Mzee Machano ni miongoni mwa Wazee ambao wametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Zanzibar katika nyanja za kiserikali na kisiasa.
Mzee Machano aliwahi kuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar (BLM) 1984 - 1985.
Kwa nafasi hii ya Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi ilimpatia fursa ya kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, lakini pia alikuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania.
Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema Mzee Machano alikuwa miongoni mwa Wajumbe wa mwanzo kabisa wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Pia Mzee Machano aliwahi kuwa Msaidizi wa Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, ambapo alikuwa ni Kamisaa wa Siasa.
Makamu wa Kwanza wa Rais amefika kumjulia hali, lakini kuvuna hekima kutoka kwa mstaafu Machano.