Mashindano ya mbio za Arusha Youth Athletics Championship kufanyika Machi 28

Mashindano ya mbio za Arusha Youth Athletics Championship{(AYAC) yanayohusisha watoto wa miaka 6 hadi 14 kufanyanyika Machi 28,2021 kwa lengo la kuongeza ushiriki wa watoto katika michezo pamoja na kukuza kizazi ambacho kitakuwa na uwelewa wa taaluma katika riadha, anaripoti Mwandoishi DIRAMAKINI (Arusha).
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha mwandaaji wa mashindano ya AYAC, Juliana Mwamsavua amesema, wamefungua dirisha la usajili wa mbio hizo ambazo zitashirikisha watoto wa shule za msingi na sekondari ambao zitawahusisha watoto 302 kutoka shule mbalimbali za Jiji la Arusha. 

Amesema, mashindano hayo ambayo wameandaa kwa kushirikiana na Chama cha Riadha Wilaya ya Arusha, mkoa na taifa ambayo yatakuwa na mbio mbalimbali ikiwemo mbio ndefu, za kati, fupi za vijiti na viunzi ambayo yatafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini hapa. 

“Tumetoa mwaliko kwa shule mbalimbali ila tunaomba watoe uthibitisho mapema, kwani wale watakowahi ndio wataweza kushiriki na tumeshaweka idadi maalum kuwa watakaoshiriki ni watoto 302 tu,”amesema Juliana.  

Amefafanua kuwa, watoto watakaoshinda katika mashindano hayo AYAC watakuwa wanadhaminiwa kwenda katika mashindano ya Afrika Mashariki, Afrika na kimataifa hivyo wazazi wawape watoto nafasi ya kushiriki fursa zilizopo katika mashindano hayo kwani kupitia michezo wanaweza kutoka kimaisha. 

“Wapeni nafasi watoto waje washiriki katika mashindano kwani riadha inachangia katika pato la taifa na hamjui baadae mtoto anaweza kuja kuwa nani, tumefungua usajili kuanzia sasa na mnaweza kutupata kupitia namba za simu 0754 623517,”ameeleza Juliana.

 Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania,John Bayo amesema, mbio za uwanjani zilikuwa hazijapewa kimpaumbele hivyo anamshukuru mwandaaji wa mbio hizo kwa kuwekeza kwa watoto ambao ndio wanariadha wa kesho japo baadhi ya shule wanafanya kwa kiasi kidogo.

Aidha, Rogath Stehen ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Riadha Mkoa wa Arusha amesema kuwa, mbio moja ni muhimu sana kwani zinalenga watoto wadogo ambazo zitakuwa na mbio nyingi za watoto ili kuhakikisha wanaendeleza vipaji vya watoto ili kuwa na mnyororo wa wanariadha ambao wakistaafu wakubwa na wao wanaendeleza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news