NGOMA AFRICA BAND YA UJERUMANI YAMLILIA HAYATI RAIS MAGUFULI

Bendi maarufu ya muziki wa dansi The Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani, wamepokea kwa masikitiko na uchungu mkubwa msiba wa kifo cha Rais John Pombe Magufuli.

Kiongozi wa bendi hiyo mwanamziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja kwa niyaba ya bendi yake anatoa pole kwa kwa Rais mpya Mama Samia Suluhu Hassan,pole kwa mama Janet Magufuli na familia yake na pole kwa watanzania wote. 

Bendi ya Ngoma Africa band inaungana na watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na kiongozi wetu Rais Magufuli ambaye alikuwa kipenzi chetu na rais aliyejitoa muanga kwa ajili ya wanyonge. 

Ngoma Africa Band inaungana na watanzania katika maombolezo ya msiba huu. 

Mungu ampumzishe Peponi Kiongozi wetu Hayati Rais John Pombe Magufuli - Ameen
MUNGU IBARIKI TANZANIA

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news