Watani wa jadi katika soka la Tanzania vilabu viwili vya Simba na Yanga vimeendelea kuonyeshana ubabe katika soka, baada ya Klabu ya Simba Queens kuibamiza klabu ya Yanga Princess mabao 3-0 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).
Mabao ya Simba yaliwekwa nyavuni kupitia kwa Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ dakika ya 30, Opa Clement Sanga dakika ya 43 kwa penalti na Mkongo Joel Bukuru dakika ya 50.
Simba Queens ambao ni mabingwa watetezi kwa ushindi huo wanapanda kileleni, wakifikisha alama 39, moja zaidi ya Yanga Princess baada ya wote kucheza mechi 15 katika ligi ya timu 12, wakati JKT Queens yenye alama 36 inabaki nafasi ya tatu.

Tags
Michezo