Timu ya Taifa, (Taifa Stars) imekamilisha mechi zake za Kundi J kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Libya, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).

Kiungo mshambuliaji wa Wydad Club Athletic ya Morocco, Simon Msuva ndiye aliyewapa shangwe Watanzania baada ya kufunga bao hilo ndani ya dakika ya 45.
Hata hivyo, licha ya mafanikio hayo Taifa Stars haijafuzu AFCON kufuatia kuzidiwa nguvu na Tunisia ikiwemo Equatorial Guinea zinazoshika nafasi mbili za kwanza na kukata tiketi ya kwenda Cameroon 2022.
Aidha, Tanzania inamaliza nafasi ya tatu kwa alama zake saba, nyuma ya Equatorial Guinea yenye alama tisa, Tunisia alama 16, wakati Libya ina alama tatu tu.