Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) imewaachisha kazi Anitha K. Shayo ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Matangazo na Rajab Juma Mohammed ambaye ni Msimamizi wa Dawati la Huduma kwa Wateja, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.
Wawili hao wameachishwa kazi ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za kushindwa kuzuia makosa kwenye tangazo la pongezi walilotoa katika Gazeti la Daily News la Machi 29, 2021

Katika hatua nyingine TSN wamesitisha huduma za mwakilishi wa kujitegemea wa matangazo, Lameck Samson