Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Vatican zimeahidi kuendelea kuhimiza amani na utulivu katika masuala yenye changamoto mbalimbali ili kuwezesha uwepo wa amani na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Baba Mtakatifu katika kuhimiza amani, utulivu na usalama duniani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) akisalimiana na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) wakati alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski jijini Dar es Salaam.
Prof. kabudi amesema kuwa Tanzania na Vatican kwa kutambua umuhimu wa amani, zimeahidi kuendelea kushirikiana katika mikutano ya Umoja wa Mataifa kuhimiza amani, utulivu na mshikamano katika masuala mbalimbali yenye changamoto kwa binadamu duniani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) akiongea na Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
“Tumeongelea umuhimu wa kulinda amani, utulivu na usalama duniani kote
hasa katika maeneo yanayokumbwa na matatizo ya vita, katika hilo pia
tuliongela suala la amani na usalama katika ukanda wa nchi za maziwa
makuu, Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika tukijua kuwa kuna maeneo
yanayohitaji amani ikiwemo eneo la kaskazini mwa Masumbiji, na mashariki
ya Demokrasia ya Kongo,”amesema Prof. Kabudi
Prof. Kabudi
ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni na hata sasa dunia
inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji mshikamano wa mataifa
yote duniani ili kuweza kuyakabili hii ikiwa ni pamoja na masuala
yanayohusu amani, utulivu, majanga, na magonjwa ya mlipuko kama vile
Covid 19, na yale yanayohusu umasikini na hali yamaisha ya watu
kubaguliwa na kuonewa.
Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczynski akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, (Mb) wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam
“Mfano katika mapambano dhidi ya Uviko
19, Vatican na Baba Mtakatifu wanayo nafasi kubwa ya kutoa mchango wao
katika eneo hilo katika kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya Covid -19
hayageuzwi kuwa katika masuala ya kibiashara na kisiasa na badala yake
mapambano hayo yazingatie utu, undugu na imani, Ameongeza Pro. Kabudi
Kwa
upande wake Balozi wa Vatican hapa Nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek
Solczynski amesema kuwa Vatican itaendelea kuimarisha mahusiano yake ya
kidiplomasia na Tanzania kwa masuala yenye maslahi ya haki, utu, amani
na utulivu.
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika MAshariki, Mhe. William Tate Ole Nasha akiongea na Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika MAshariki, Mhe. William Tate Ole Nasha wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam .
“Maongezi yangu na Mhe. Waziri yalikuwa mazuri kwani
tuliongelea masuala mbalimbali yenye maslahi kwa binadamu yakiwemo
masuala ya kukuza diplomasia yetu pamoja na masuala ya amani na usalama
duniani,”amesema Askofu Mkuu Solczynski.
Baba Mtakatifu Papa
Francisko alimteua, Askofu Mkuu Marek Solczyński kuwa Balozi mpya wa
Vatican nchini Tanzania mwezi Aprili, 2017. Kabla ya uteuzi huu, Askofu
mkuu Solczyński alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Georgia, Armenia na
Azerbaijan.
Katika tukio jingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Tate Olenasha amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria hapa nchini Mhe. Ahmed Djellal ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu kuimarisha diplomasia baina ya Tanzania na Algeria.
Tags
Kimataifa