Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka amewaomba wadau na wananchi wa mkoa Kagera kuendelea kuichangia timu ya Nyaishozi FC ambao ni mabingwa wa ligi Mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo imepagwa kundi D na itachezea mechi katika kituo cha Katavi,anaripoti Eliud Rwechungura (Karagwe).
Mheruka ameyasema leo,Machi 1, 2021 alipokuwa akipokea jezi za wachezaji na pesa ya kuisaidia timu kutoka kwa Kampuni ya Hlucky Kombucha Investment ambao ni wazalishaji wa kinywaji cha Kombucha Ginger Drink ambao ni wadhamini wa timu ya Nyaishozi FC.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka (kulia) akipokea jezi kutoka Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha Investment, Bw. Hamis Jumanne ambao ni wadhamini wa timu ya Nyaishozi FC mabingwa wa ligi mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo itachezea mechi katika kituo cha Katavi imepagwa kundi D, nyuma ni kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Karagwe Kagera, Leo, Machi 01, 2021.
‘‘Nitoe wito kwa Wananchi wote na wadau waendelee kuichangia timu yetu Nyaishozi, Timu hii imetutoa kimaso maso ni timu ambayo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Kagera lakini pia niwashukuru umoja wa Wanakaragwe wanaoishi Dar es salaam nao wanaendelea kufanya michango yao kupitia WhatsApp pia Jambo Bukoba ambao tumeshapokea michango yao,”amesema.
Mheruka ameendelea kumpongeza Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha Investment, Bw. Hamis Jumanne ambae amekuwa mstali wa mbele kwa kujitoa kuiwezesha timu hiyo pia kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya wilaya Karagwe pia ameonekana akiandaa matamasha mbalimbali ya kutafuta na kuinua vipaji vya vijana ndani ya wilaya Karagwe.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha investment, Bw. Hamis Jumanne amesema kuwa Kampuni yake imeamua kuunga mkono timu ya Nyaishozi FC ili kuunga mkono michezo ndani ya mkoa lakini pia kuumunga mkono Rais wetu pia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ndie Mbunge wa Jimbo la Karagwe kwa sababu tuna timu ambayo imewakilisha wilaya Karagwe vizuri na sasa inaendelea kuuwakilisha Mkoa vizuri katika ligi ya Mikoa (RCL2021). Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka (kulia) akipokea kiasi cha pesa kutoka Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha Investment, Bw. Hamis Jumanne ambao ni wadhamini wa timu ya Nyaishozi FC mabingwa wa ligi mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo itachezea mechi katika kituo cha Katavi imepagwa kundi D, nyuma ni kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Karagwe Kagera leo, Machi 1, 2021.
Aidha, Bw. Hamis Jumanne ameendelea kuihakikishia timu ya Nyaishozi
FC kuwa atakuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na wananchi na wadau
wengine kuunga mkoa timu hiyo ili iweze kushinda katika ligi ya mikoa
ili hata wilaya ya Karagwe tupate hata timu ya Kutuwakilisha katika ligi
Daraja la pili panapo majaliwa.
Naye, Kocha Msaidizi wa timu ya
Nyaishozi Fc, Jonson Majara amewahakikishia wananchi wa wilaya ya
Karagwe na mkoa wa Kagera kuwa tayali timu ipo kambini na imeshajipanga
vizuri kwa kushirikiana na benchi la ufundi na uongozi wa timu
kuhakikisha inarudi na ushindi ili angalau mkoa upate timu ya pili
inayocheza ligi katika daraja la juu, itapendeza sana kwasababu timu hii
ni timu ya wanannchi ukizingatia namna ambavyo wanaendelea kujitoa kwa
ajili ya timu hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha Investment, Bw. Hamis Jumanne akiwa katika picha pamoja na Katibu Msaidizi wa msaidizi wa Chama cha mpira mkoa Kagera, Majaliwa Said na Kocha Msaidizi wa timu ya Nyaishozi Fc, Jonson Majara mara baada ya kukabidhi jezi ya pesa za kusaidia timu ya Nyaishozi FC mabingwa wa ligi mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo itachezea mechi katika kituo cha Katavi imepagwa kundi D, Karagwe Kagera leo, Machi 01, 2021.Awali, Katibu Msaidizi wa msaidizi wa Chama cha mpira mkoa Kagera, Majaliwa Said amewashukuru wananchi na wadau wote wanaoendelea kujitoa na kuunga mkono timu ya Nyaishozi maana timu bado ni changa kushiriki ligi hizi na amehaidi atashirikiana na timu kuhakikisha inapata ushindi katika ligi hiyo inayoanza Machi 04, 2021 huko mkoani Katavi.