TSC waadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa ufanisi

Wafanyakazi wanawake wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Makao Makuu Dodoma, wameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa ufanisi,anaripoti Veronica Simba (TSC).
Wafanyakazi wanawake wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Makao Makuu Dodoma, wakishiriki katika maandamano wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, 2021.
Wafanyakazi wanawake wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Makao Makuu Dodoma, wakishiriki katika maandamano wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, 2021.

Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika leo, Machi 8, 2021 jijini Dodoma, Wafanyakazi hao wameshiriki katika maandamano yaliyoshirikisha Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi, yaliyoanzia Uwanja wa Jamhuri hadi katika Uwanja wa ‘Nyerere Square.’

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wanawake wa TSC, Mwenyekiti wao, Catherine Kamili ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwathamini wanawake na kuwapatia nafasi za uongozi katika nyanja mbalimbali nchini. Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), wakiungana na wenzao kutoka Taasisi mbalimbali kucheza, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa ‘Nyerere Square’ jijini Dodoma, Machi 8, 2021.
Wafanyakazi wanawake wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Makao Makuu Dodoma, wakiwa katika picha ya pamoja, muda mfupi kabla ya kushiriki katika maandamano wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, 2021.

Aidha, amewataka wanawake wote nchini, hususani watumishi wa TSC, kuendelea kuchapa kazi kwa weledi na kujituma katika kuhakikisha, wanakuwa sehemu ya waleta maendeleo ya jamii na Taifa.

Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kitaifa, mwaka huu ni “Wanawake katika Uongozi, Chachu kufikia Dunia yenye Usawa.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news