Tume ya Utumishi wa Umma imepanga kufanya Mkutano wa Tatu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kuanzia Machi 15 hadi 26, 2021, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).
Hayo yamebainishwa leo Machi 12, 2021 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Tume ya Utumishi wa Umma, Richard M.Cheyo kupitia taarifa aliyoitoa kwa umma.
Amesema, katika mkutano huo Tume itapokea na kutolea uamuzi Rufaa 99 na Malalamiko sita yaliyowasilishwa na Watumishi mbalimbali wa Umma, ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka zao za Nidhamu.
"Shughuli nyingine iliyopangwa kufanyika wakati wa Mkutano huu ni pamoja na kupokea na kujadili, taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma katika kipindi cha Robo ya Pili (Oktoba hadi Disemba, 2020) ya mwaka wa fedha 2020/2021,"amefafanua Cheyo.
Tume ya Utumishi wa Umma inatekeleza majukumu haya kwa mujibu wa Kifungu cha 10(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298.
Tags
Habari