Tume ya Utumishi wa Umma yaahirisha mkutano

Kufuatia msiba wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Joseph Magufuli uliotokea Machi 17, 2021 Tume ya Utumishi wa Umma imeahirisha vikao vyake vya Mkutano wa Tatu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 uliokuwa umeanza kufanyika Machi 15 hadi Machi 17, 2021, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Tume ya Utumishi wa Umma,Richard M.Cheyo.

Ameeleza kuwa, ratiba na tarehe ya kuendelea kufanyika kwa mkutano huo wa kupokea na kutolea uamuzi rufaa na malalamiko yaliyowasilishwa Tume na watumishi mbalimbali wa umma,ambao hawakuridhikana uamuzi uliotolewa na waajiri,mamlaka za ajira na nidhamu katika utumishi wa umma itatolewa hivi karibuni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news