UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO:TAREHE: 12/03/2021.
Mikoa ya Kigoma, Katavi, Kagera na Geita inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.........
Mikoa ya Njombe na Ruvuma inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, Mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.........
Mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.........
Mikoa ya Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Iringa, Dodoma, Singida, Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Manyara, Arusha, Visiwa vya Unguja na Pemba,Mtwara na Lindi inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
.........
KIWANGO CHA JUU CHA JOTO NI NYUZI JOTO 35 ( 35°C ) KATIKA MAENEO YA KILIMANJARO NA MOSHI.
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani yote; Kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini na kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Madogo hadi Makubwa kiasi.
Matarajio kwa siku ya Jumapili tarehe 14/03/2021: Mabadiliko kidogo
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 12/03/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
Tags
Habari