UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 03/03/2021.
Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa, Rukwa, Njombe, Ruvuma pamoja na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
.......................
Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Kigoma, Tabora, Katavi, Mtwara na Lindi: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
........................
Mikoa ya Dodoma, Singida pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
.......................
Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
........................
Mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na Arusha: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
........................
ANGALIZO:
VIPINDI VYA UPEPO MKALI UNAOFIKIA KM 40 KWA SAA NA MAWIMBI MAKUBWA YANAYOFIKIA MITA 2 VINATARAJIWA
KATIKA BAADHI YA MAENEO YA UKANDA PWANI YA BAHARI YA HINDI (MIKOA YA LINDI, MTWARA, TANGA, DAR ES SALAAM NA PWANI (IKIJUMUISHA VISIWA VYA MAFIA) PAMOJA NA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA).