Bosi wa Manchester United ya England ajiuzulu

Edward Gareth Woodward ambaye ni mtendaji mkuu wa klabu ya Manchester United ya England amejiuzulu wadhifa huo baada ya kuwa mmoja wa viongozi waliohusika kwenye wazo la kuanzishwa wa European Super League (ESL).
Edward Gareth Woodward. (Picha na Gettyimages).

Kujiuzulu kwake kumekuja baada ya shinikizo kubwa kutoka mashabiki wa vilabu sita ambavyo ni Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham, kuandamana wakishinikiza vilabu hivyo kutoshiriki kwenye michuano hiyo barani Ulaya.

Awali Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) ilitoa onyo kali kwa wachezaji ambao wangeshiriki ligi hivyo wasingepata vibali vya kucheza kwenye timu zao za taifa kwenye michuano ambayo inasimamiwa na shirikisho hilo.

Aprili 20,mwaka huu mchezo kati Chelsea dhidi ya Brighton ambao uliisha kwa sare ulilazamika kuchelewa kuanza kwa dakika 40 baada ya mashabiki kufurika nje wa uwanja wa Stamford Brigde wakishinikiza klabu hiyo kuachana na mpango huo.

Kwani mpango huo ulionekana una lengo la kuzinufaisha timu hizo kubwa na kuweka rehani uhai wa timu ndogo na zakati ambazo hazina fedha nyingi barani Ulaya.



Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news