Halmashauri Kuu ya CCM yampitisha Rais Samia kwa asilimia 100 mgombea pekee Uenyekiti CCM

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema Halmashauri Kuu ya CCM imempitisha Mjumbe wa Kamati Kuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kwa asilimia 100 kuwa mgombea pekee wa nafasi ya mwenyekiti ndani ya chama hicho, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dodoma).

Polepole ameyasema hayo leo jijini Dodom ambapo amesema uteuzi huo ni kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyefariki Machi 17, mwaka huu akiwa katika matibabu katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam na kuzikwa Aprili 26, mwaka huu huko nyumbani kwake wilayani Chato, Geita

Mheshimiwa Polepole amesema, kwa mujibu wa Katiba ya CCM nafasi ya Mwenyekiti ipo wazi na inatakiwa kujazwa kupitia Ibara ya 99.

Amesema, Halmashauri Kuu imewapitisha wajumbe watatu ambao watasimamia uchaguzi huo akiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu, Job Ndugai,Mjumbe wa Baraza la Wawalishi, Zuberi Maulid na Mjumbe wa Kamati Kuu, Gaundensia Kabaka .

Amesema, mkutano huo hautakuwa na burudani wala shangwe na nderemo kama ilivyo desturi kunapofanyika Mkutano Mkuu kutokana na chama kuwa bado kipo kwenye majonzi ya kumpoteza aliyekuwa mwenyekiti nwake, Hayati Dkt. Magufuli na badala yake kutaimbwa nyimbo mbili kutoka bendi ya chama hicho.

Polepole amesema,kwa kauli moja Halmashauri kuu Taifa ina imani kubwa na Samia Suluhu Hassan kutokana na uaminifu, uzalendo ,uadilifu na mapenzi mema juu kwa CCM.

Rais Samia anatarajiwa kuthibitishwa kuwa Mwenyekiti wa CCM kesho Aprili 30, mwaka huu na wajumbe 1,876 wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news