KMC WAENDELEA KUJIFUA KUELEKEA KWENYE MCHEZO DHIDI YA YANGA JUMAMOSI

Kikosi cha KMC FC kinaendelea kujifua kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara dhidi ya Yanga ukataopigwa siku ya Jumamosi ya Aprili 10 katika uwanja wa Mkapa saa moja kamili jioni (19:00).
Goli Kipa wa Timu ya KMC FC Sudi Dondola akiwa kwenye mazoezi ya kujifua kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga hapo Jumamosi.
wachezaji wa Timu ya KMC FC wakiwa kwenye mazoezi.
Kocha Mkuu wa Timu ya KMC FC , John Simkoko akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Timu hiyo katika mazoezi ambayo KinoBoys wanaendelea nayo hivi sasa.

Katika mchezo huo KMC FC inakutana na Yanga kwa mara ya pili huku ikiwa ugenini kwenye msimu huu wa Ligi Kuu 2020/2021 umejipanga kuhakikisha kwamba inaleta furaha kwa mashabiki na kwamba wajitokeze uwanjani kutoa sapoti kwa wachezaji kwani Kino Boys inakwenda kupambania alama tatu muhimu kwenye mchezo huo.

KMC FC inatafuta ushindi huo ili kujiimarisha katika msimamo wa ligi Kuu na kwamba licha ya kuwa na upinzani mkubwa wakupambania alama tatu lakini bado mchezo huo upo ndani ya Timu ya Manispaa ya Kinondoni na kwamba hakuna kitakachoshindikana.

“Tunakwenda kwenye mchezo ambao kimsingi hautakuwa mwepesi kutokana na aina ya timu ambayo tunakutana nayo, ni nzuri, wanafanya vizuri, lakini pia wanaongoza ligi, hivyo mchezo utakuwa mgumu lakini pamoja na yote bado KMC FC tunasema kwamba tunakwenda kupambanania alama tatu na tunaimani kubwa yakufanya vizuri kwenye mchezo wetu.

Katika msimuu huu KMC FC ilikutana na yanga Oktoba mwaka jana katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na kupoteza mchezo huo ambapo walifunga magoli mawili kwa moja, Goli la KMC lilifungwa na Hassan Kabunda kipindi cha kwanza katika dakika ya 23.

Imetolewa na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mahusiano wa Timu ya KMC FC

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news