Imebainika kuwa kuna idadi kubwa ya Mawakili ambao mpaka kufikia tarehe ya tangazo hili hawajahuisha taarifa zao binafsi na kuweka maelezo muhimu katika akuanti zao kwenye mfumo wa mawakili Tanzania unaojulikana kama Tanzania Advocate Management System (TAMS). Mawakili hawa wako wapi,kumepelekea kutokuwepo taarifa zao kwenye mfumo wa Mawakili Tanzania pamoja na Kanzidata ya Mawakili. Aidha, uwepo wa taarifa sahihi za Wakili anayehusika katika Chama cha Wanasheria Tanganyika na Ofisi ya Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kunawapa fursa wadau wote na wananchi kwa ujumla kuwafahamu Mawakili walioruhusiwa kufanya kazi ya Uwakili, hivyo kama Mahakama ya Tanzania kupitia Ofisi ya Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania inauntangazia umma kwamba mtu yeyote ambaye ana taarifa za Wakili au anafahamu chochote kuhusu yeyote aliyeorodheshwa katika orodha iliyowekwa hapa chini tafadhali anaombwa kutoa taarifa hizo kupitia anuani ya barua pepe rhc@judiciary.go.tz au unaweza kupiga simu ya mkononi nambari 0739303038. Kwa maelezo zaidi kuhusu tangazao la 'Mawakili Wasiojulikana' tafadhali tembelea tovuti yetu www.judiciary.go.tz na kwenye blogu yetu Tanzaniajudiciary.blogspot.com.
Tags
Tangazo
Mr. Kassian mussa nkwera
ReplyDelete