Makamu wa Kwanza wa Rais Mheshimiwa Othman Masoud Othman asisitiza kuwatumikia wote bila kujali itikadi za vyama vya siasa

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman ameahidi kuwatumikia wananchi wa Zanzibar bila ya kuangalia itikadi za vyama vyao vya siasa, anaripoti Mwandishi Diramakini (Zanzibar).
"Najua kila mtu hapa ana utamaduni wake na chama chake cha siasa, lakini kwangu mimi katika kuwatumikia naitanguliza mbele Zanzibar na maslahi ya Wazanzibari wenyewe,"amefafanua.

Makamu wa Kwanza wa Rais ameyasema hayo wakati akiendelea na ziara yake ya kuangilia wagonjwa na wananchi wenye matatizo mbalimbali kutoka Mkoa wa Kusini Unguja.
Mheshimiwa Othman amewaahidi wananchi hao kwamba ataendelea na utaratibu huo wakurudi kwao mara kwa mara na kubadilishana nao mawazo, kama ilivyokuwa desturi ya mtangulizi wake Marehemu Maalim Seif.

Nae Sheha wa Shehia ya Tasini Makunduchi Bwana Juma Ali Khatib, amesema utaratibu huu wa viongozi kushuka chini kwa wananchi ni mzuri sana kwao, kwani utasaidia kutatua matatizo yao mengi ambayo wananchi hao wanakumbana nayo.
Aidha Sheha huyo amewataka zaidi wananchi wake kuwa wawazi kueleza matatizo yao pindi watakapokuwa wanapata fursa za kukutana na viongozi wakuu wa kiserikali.
Baadhi ya wananchi wa mkoa wa kusini wametowa maombi yao kwa viongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar kwakusema hali ya amani iliyopo sasa nchini ni nzuri, hivyo wamewaomba viongozi kuidumisha hali hiyo hata nyakati za uchaguzi.

Wananchi 12 kutoka katika majimbo ya mkoa wa Kusini Unguja,wamepata fursa ya kutembelewa na kiongozi huyo pamoja na kupatiwa sadaka ya futari amabayo itawasaidia kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news