Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud aendelea kutoa faraja kwa makundi mbalimbali ya jamii jijini Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud, amewataka wananchi wa mkoa wa Kaskazini Unguja kujenga umoja na mshikamano ili kutoa fursa kwa serikali kupambana katika kuleta maendeleo.Makamu wa kwanza ameyasema hayo mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kutembelea baadhi wagonjwa na wananchi wenye matatizo mbalimbali waliomo katika mkoa wa huo wa kaskazini Unguja.
Mheshimiwa Othman amesisitiza kwamba kama alivyoirithi nafasi ya Umakamu wa kwanza kutoka kwa mtangulizi wake Marehemu Maalim Seif, basi atahakikisha anawatumikia vyema Wazanzibari ili kuhakikisha Zanzibar inapiga hatua.
"Lengo letu kama serikali ni kupiga hatua zaidi na kutoka hapa tulipo na kusogea mbele, tena tusogee mbele zaidi panapostahiki, na katika kulifikia hili niwajibu wetu kwa pamoja kushirikiana kuhakikisha hili linafanikiwa,"amefafanua.

"Umoja na mshikamano ukikosekana katika jamii maendeleo pia hayatakuwa na nafasi, hivyo ni jukumu letu kama Wazanzibari kuungana na kuwa kitu kimoja kwa maslahi yetu wote,"ameongeza.
Aidha, Mheshimiwa Othman alisema hatoyaangusha matumaini ya Wazanzibari juu yake kwakusisitiza kuendeleza juhudi zilizoanzishwa.

"Kwa yale yote yaliwakuwa yameanzishwa na yale ambayo tunayahitajia kuyaimarisha zaidi, mimi Makamu wa kwanza wa Rais nachukua dhamana na nitahakikisha kwa juhudi na maarifa yangu inshaallah nitawatumikia Wazanzibari na tutafikia malengo,"ameeleza Mheshimiwa Othman.
Wakazi wa maeneo mbalimbali katika mkoa wa Kaskazini Unguja wamekishukuru kitendo hicho cha Makamu wa kwanza wa Rais, kushuka chini na kuwafariji wananchi wake wakisema kwamba wanaiona thamani yao mbele ya viongozi hao wakuu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news