Marekani yaahidi kuleta neema za maendeleo Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais atoa neno

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema Serikali ya Zanzibar ipo tayari kuendelea kuimarisha mahusiano yake na nchi ya Marekani ili kufikia malengo ya kimaendeleo Zanzibar, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mheshimiwa Othman ameyasema hayo mara baada ya kukamilisha mazungumzo na mgeni wake Bwana Donald Wright, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Aprili 27, 2021 ofisini kwake jijini Zanzibar.

Balozi Donald alifika Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Migombani Unguja, kwa lengo la kujitambulisha sambamba na kuimarisha mahusiano mema kati ya nchi hizo mbili.

"Lengo la ujio wetu kwa serikali ya Zanzibar ni kuendelea kuimarisha mahusiano yetu ya muda mrefu, lakini suala la afya, biashara na kutoa elimu kwa wananchi juu ya utumiaji wa fursa zilizopo katika utalii ni miongoni mwa vipaombele vitatu ambavyo tunategemea kuvitekeleza ili kuisaidia Zanzibar," ameeleza Balozi Donald.




Nae Makamu wa Kwanza wa Rais, alimshukuru Balozi Donald kwa kwaniaba ya nchi ya Marekani kwa namna ambavyo inaendelea kuisaidia Zanzibar.

"Marekani ni nchi rafiki na ina mchango mkubwa kwa Visiwa vyetu vya Zanzibar, kwani itakumbukwa kwamba ilishawahi kutusaidia miradi mbali mbali,kama vile mradi wa kupiga vita malaria, mradi wa umeme pamoja na barabara katika kisiwa cha Pemba ambazo zilikuwa chini ya mradi wa MCC," alifafanua Makamu huyo wa kwanza.

Makamu wa Kwanza amemtaka Balozi kuendelea kuitembea Zanzibar, na muda wowote anakaribishwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news