Nafasi ya tatu katika Msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara inashikiliwa na Wekundu wa Msimbazi, Simba SC kwa alama 49, ANARIPOTI MWANDISHI DFIRAMAKINI.
Aidha, wanatarajiwa kucheza na Mwadui FC mjini Shinyanga ambapo tayari wamecheza mechi 21 katika msimamo huo.
Simba ambayo ilikuwa kwenye majukumu ya kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, ilirejea wiki iliyopita na kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar na kushinda bao 5-0.
Kwa mujibu wa tovuti ya Simba imeandika kuwa Kocha Didier Gomez na wasaidizi wake, wameamua kuondoka na kikosi kizima kutokana ugumu wa mechi huku timu zote zikiwa zimejipanga kipindi hiki cha lala salama ligi ikielekea ukingoni.
Ratiba ya michezo hiyo Kanda ya Ziwa itaanza leo Jumapili ambapo itashuka kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga kuikabili Mwadui na siku tatu baadaye yaani Jumatano itacheza na Kagera Sugar Kaitaba kabla ya kumalizana na Gwambina Aprili 24.
Kikosi Kamili kilichopo Kanda ya Ziwa;
Makipa:- Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim
Mabeki:-Shomari Kapombe, Joash Onyango, Pascal Wawa, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Mohamed Hussein, Kennedy Juma, David Kameta
Viungo:Jonas Mkude, Rally Bwalya, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Luis Miquissone, Hassan Dilunga, Clatous Chama, Bernard Morrsion, Francis Kahata, Taddeo Lwanga.
Washambuliaji:Medie Kagere, John Bocco, Ibrahim Ajib, Kope Mugalu, Miraji Athumani, Perfect Chikwende.TAZAMA CHINI LIVE