Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepongeza utayari wa mabalozi kutoka nchi za Marekani, Ufaransa na Switzerland wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar kiuchumi na kimaendeleo, anaripoti Mwandishi Maalum DIRAMAKINI (Zanzibar).
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Aprili 27, 2021 kwa nyakati tofauti wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Donald John Wright, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier pamoja na Balozi wa Switzaland nchini Tanzania, Didier Chassot, Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiania na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe.Frederic Clavier kwa kugonganisha mikoni alipowasili katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 27-4-2021.(Picha na Ikulu).
Mabalozi hao wote wametumia fursa hiyo kwa kumpongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa ushindi wake mkubwa alioupata katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2020 na kumuweza kuiongoza Zanzibar chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo imeanza kupata mafanikio makubwa.
Mabalozi hao wameeleza matarajio yao makubwa ya Zanzibar kuimarika kiuchumi, kisiasa na kijamii chini ya uongozi wa Rais Dkt.Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mgeni wake Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe. Frederic Clavier, wakitoka katika ukumbi wa baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Katika mazungumzo kati yake na Balozi wa Marekani, Donald John Wright, Rais Dkt.Mwinyi amempongeza Balozi huyo kwa azma yake ya kuiunga mkono Zanzibar hasa katika kuimarisha sekta ya afya.
Rais Dkt.Mwinyi amesema kuwa, miongoni mwa vipaumbelea ilivyoweka Serikali anayoiongoza ni pamoja na kuimarisha sekta ya afya hivyo hatua hizo za Marekani za Marekani ni chachu katika kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wa sekta ya uwekezaji, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kwamba azma ya Marekani kuleta wawekezaji pamoja na kampuni za uwekezaji katika sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya utalii kutazidi kuimarisha uchumi wa Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe. Frederic Clavier (kulia kwa Rais) akiwa na ujumbe wake, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 27-4-2021.(Picha na Ikulu). Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe. Frederic Clavier, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbiu wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi alieleza kwamba, hatua na utayari wa Marekani wa kuendeleza ushirikiano katika sekta ya biashara na viwanda kutasaidia hasa kuweza kukuza soko la ajira kwa vijana wa Zanzibar.
Nae Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Donald John Wright ameeleza malengo ya nchi yake ya kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, uwekezaji, biashara na nyinginezo.
Aidha, Balozi Wright akiwa na ujumbe wake amemueleza Rais Dkt.Mwinyi kwamba Marekani inathamini juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali anayoiongoza na kueleza kwamba nchi yake iko tayari kuziunga mkono kwani zinaonesha mwanga wa maendeleo kwa Zanzibar na wananchi wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania Mhe.Didier Chassot, alipowasili katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo na kujitambulisha na (kulia kwake) Afisa wa Ubalozi Bi. Esther Majani.(Picha na Ikulu).
Rais Dkt.Mwinyi pia, amefanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier ambapo Balozi huyo aliahidi kuiunga mkono Zanzibar katika mikakati yake ya kuimarisha uchumi wa buluu.
Aidha, Balozi Clavier ameeleza hatua atakazozichukua katika kuhakikisha wawekezaji pamoja na wafanyabiashara wa Ufaransa wanakuja kuekeza Zanzibar katika sekta mbalimbali zilizopo ikiwemo sekta ya utalii.
Balozi Clavier pia, alitumia fursa hiyo kumueleza Rais Dkt.Mwinyi azma ya nchi yake kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya nishati, kilimo, usafiri na usafirishaji, uhifadhi wa mazingira pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutoa mafumzo mbalimbali ya ujasiriamali. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Katika mazungumzo hayo, Balozi Clavier akiwa na ujumbe wake walimuahidi Rais Dkt.Mwinyi kwamba Ufaransa ina mpango wa kuikutanisha Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenye Viwanda ya Zanzibar pamoja na ile ya Ufaransa ambazo zitakutakana katika mkutano maalum uliotayarishwa na Ubalozi huo.
Pia, ubalozi huo umeeleza azma ya kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika sanaa, lugha pamoja na mashirikiano kwa vyuo vikuu kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na utaalamu kati ya Vyuo Vikuu vya Zanzibar na Ufaransa.
Nae Rais Dkt.Mwinyi kwa upande wake aliipongeza Ufaransa kwa azma yake hiyo na kueleza kwamba sekta zote ambazo imeahidi kuiunga mkono Zanzibar tayari Zanzibar imeshazipa kipaumbele hivyo juhudi hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa katika kufikia lengo lililokusudiwa. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na mgeni wake Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbui wa Ikulu Jijini Zanzibar alipofika kujitambulisha.(Picha na Ikulu) .
Aidha, alimueleza Balozi huyo mikakati iliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha uchumi wake unaimarika na wananchi wake wanapata maendeleo ikiwa ni pamoja na kuifanya Pemba kuwa ni sehemu maalum ya uwekezaji sambamba na kuiwekeza mazingira mazuri ya uwekezaji
Wakati huo huo, Rais Dkt. Mwinyi alikutana na Balozi wa Switzerland nchini Tanzania, Didier Chassot, ambapo katika mazungumzo yao viongozi hao waliahidi kuendeza ushirikiano uliopo hasa katika sekta ya afya ambapo nchi hiyo imeahidi kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Sambamba na hayo, Balozi huyo wa Switzerland alieleza hatua ambazo itazichukua nchi yake katika kuiunga mkono Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwajengea uwezo pamoja na mafunzo kwa vijana ili kukuza ubunifu na hatimae waweze kujiari wenyewe.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Mhe.Donald John Wright, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha mazungumzo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Mhe. Donald John Wright alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 27-4-2021, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Mhe.Donald John Wright, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha,mazungumzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo.27-4-2021.(Picha na Ikulu).
Balozi Chassot pia, alimueleza Rais Dkt. Mwinyi azma Switzerland ya kuiunga mkono Zanzibar kwa kusaidia wataalamu wa Bima ya Afya pamoja na kuiimarisha Taasisi ya Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) ili kumpa nguvu Rais katika juhudi zake za kupambana na rushwa.
Rais Dkt.Mwinyi kwa upande wake alimpongeza Balozi Chassot kwa azma ya serikali yake ya kuiunga mkono Zanzibar katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo sekta ya afya, kuwajengea uwezo vijana katika sekta ya ajira, kupambana na rushwa pamoja na kuwaendeleza akina mama mambo ambayo yote hayo yamepewa kipaumbele na Serikali anayoiongoza.
Sambamba na hayo, Rais Dkt.Mwinyi aliwaeleza mabalozi hao kwamba Wazanzibari kuwa kitu kimoja kwa kushirikiana katika Serikali yao ya Umoja wa Kitaifa kutaendeleza umoja, amani, mshikamano sanjari na maendeleo endelevu kwa nchi na wananchi wake.
Tags
Habari