MWALIMU MAKURU LAMECK JOSEPH AWAPA NENO WABUNGE WA MKOA WA MARA

Wabunge wa Majimbo ya Mkoa wa Mara wameombwa kuzidi kuusemea Mkoa wao na changamoto zilizomo ndani ya Mkoa huo hatua ambayo itawezesha Serikali kuchukua hatua madhubuti za kuzitatua kwa maslahi mapana ya Wananchi, anaripoti Amos Lufungilo (DIRAMAKINI) Mara.

Pia, wameaswa kuwa kiungo madhubuti katika kushirikiana na Viongozi wa Serikali na Wananchi katika majimbo yao.katika kusikiliza changamoto za Wananchi na kuweka mikakati thabiti ya ufumbuzi wake, ambapo kwa kufanya hivyo Maendeleo yatazidi kutekelezeka kwa ufanisi na kuzidi kukifanya chama Cha Mapinduzi kuendelea kuaminika Kama ilivyo sasa na kuendelea.

Hayo yamebainishwa na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma Mjini, Mwalimu Makuru Lameck Joseph wakati akizungumza na DIRAMAKINI Mjini Musoma. Ambapo pamoja na mambo mengine, amewasisitiza Wabunge wa Mkoa huo kuwa sauti ya Wananchi wawapo Bungeni kwa kuwawakilisha kikamilifu ikiwemo kuwathilisha changamoto zao na kuiomba Serikali kuzitatua Kutokana na dhamana waliyonayo.

"Bahati kubwa Wabunge wote wanatokana na Chama Cha Mapinduzi ambao ndio wawakikishi wetu. Katika uongozi wa Hayati Dokta Magufuli, yapo Maendeleo makubwa Sana yamefanyika katika Mkoa wetu ambayo kim-singi ni alama ya kukumbukwa na vizazi vijavyo. Maendeleo hayo yalipatikana kwa miaka 5 ya uongozi wake ambapo Majimbo mengine yalikuwa na Wabunge Kutoka vyama vya upinzani, kwa Sasa Wabunge waliopo wote wanatokana na CCM niwaombe wazidi kuzisemea changamoto zilizopo ndani ya Mkoa kwa umoja wao wanapokuwa Bungeni." amesema Mwalimu Makuru.

"Zipo changamoto za barabara ndani ya Mkoa wa Mara 'TARURA' imekuwa ikitengewa fedha kidogo kuzikarabati mambo Kama haya wanapaswa kuyasemea kusudi iongezewe fedha kuzikarabati na kuzijenga. Pia zipo barabara chini ya TANROADS ipo barabara ya lami inayojengwa kutoka Musoma Kwenda Mugumu Kupitia Butiama imekaa muda mrefu waisemee kusudi bajeti itolewe ili ujenzi ufanyike, barabara ya Tarime- Mugumu Kupitia Nyamwaga na Nyamongo itengewe fedha za kutosha kwani itarahisisha usafirishaji na kuimarisha uchumi wa wananchi,"amesema.

Aidha amewaomba Wabunge wote, kuungana kwa pamoja kuiomba Serikali kuwezesha ukamilishaji wa barabara kutoka Musoma Mjini kwenda Busekela Musoma Vijijini itengewe fedha za kutosha ikamilike mapema, kuwezesha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali na Samaki ambao kwa kiwango kikubwa huvuliwa Musoma Vijijini na kusafirishwa kupelekwa maeneo mbalimbali Nchini. hivyo uchumi wa Wananchi utaimarika na kukua kwa Kasi kubwa.

Mwalimu Makuru ameongeza kuwa, Miradi mingine wanapaswa kuiomba Serikali ilete kwa ajili ya kukuza Uchumi wa Mkoa na Maendeleo ya Wananchi wake hasa Miradi ya Maji vijijni ambako Wananchi baadhi ya maeneo wanakabiliwa na ukosefu wa huduma ya Maji Safi hali ambayo huwafanya Wananchi watumie muda mwingi kutafuta huduma.

"Wapo baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Mara wamekuwa na utaratibu mzuri wa kufanya mikutano ya hadhara na kupokea kero za Wananchi na kuzipeleka Bungeni, jambo hili ni zuri Sana na linawapa Wananchi fursa ya Kuwa huru kueleza changamoto zao na kijua Serikali itazitatua vipi. Naomba Wabunge wote wajiwekee utaratibu huu na wawe na ushirikiano na Wananchi wao na Viongozi wa ngazi za Halmashauri pasipo kwa kuwatumikia Wananchi wote."amesema Mwal Makuru.

Ameongeza Kuwa, Mkoa wa Mara unaheshimika kitaifa na Kimataifa kwani ulimtoa kiongozi shupavu na Mwasisi wa Taifa la Tanzania. Hivyo akasema iwapo Wabunge watazingatia kutekeleza wajibu wao kwa kuiomba Serikali kuja kuzidi kuleta Maendeleo litakuwa Jambo la heshima.

Aidha Mwalimu Makuru amewaomba Watanzania kwa ujumla, kuendelea kuchapa kazi kwa bidii huku wakimtanguliza Mungu pamoja na kuiombea Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan iweze kuwatumikia kwa ufanisi huku akisisitiza umoja, upendo na mshikamano udumishwe kwa maslahi ya Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news