Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, ujenzi wa jengo jipya la abiria (Terminal III) katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume unapaswa kwenda sambamba na utoaji wa huduma bora kwa wasafiri, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Zanzibar).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali baada ya kumaliza ziara yake kutembelea jengo jipya la Abiria la Terminal 3 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani
Karume, wakati alipolitembelea Jengo jipya la Abiria (Terminal III)
lililo katika hatua za mwisho kukamilika ujenzi wake.
Amesema,
ujenzi wa jengo hilo umefanywa ili kuimarisha upatikanaji wa huduma bora
kwa wasafiri, hivyo akawataka wasimamizi wa ujenzi kuhakikisha kasoro
mbalimbali zilizopo katika jengo hilo zinarekebishwa ili kuwepo utoaji
mzuri wa huduma.
Rais Dkt.Mwinyi alisema kuwa, ameridhishwa na
hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo na kuwataka wasimamizi wa ujenzi
kurekebisha mapungufu madogo madogo ili kuwa na uwanja wa kisasa na
kuepuka hali iliyopo katika jengo la zamani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea jengo jipya la Abiria la Terminal 3 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi.Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea jengo jepya la Abiria la Terminal 3 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,akimsikiliza Msimamizi wa Ujenzi wa Serikali wa jengo hilo Mhandisi Yassir De Coster wakati wa ziara yake leo 14—4-2021.(Picha na Ikulu).Aliyataja maeneo
yanayohitaji kushughulikiwa kuwa ni pamoja na kuongeza vizimba vya
Uhamiaji, eneo la ukaguzi wa mizigo pamoja na kuongeza mashine kwa
watendaji wa masuala ya‘Custom’.
Dkt. Mwinyi aliwataka wasimamizi
wa ujenzi huo kuhakikisha kunakuwepo mabango yanayoainisha taarifa za
safari za ndege,kama ilivyo katika viwanja vyote vya Kimataifa Duniani,
jambo ambalo halijafanyika hadi hivi sasa.
Aidha, aliwataka
kukamilisha hatua mbali mbali zilizobaki mbele ya jengo hilo, ikiwemo
upandaji wa majani, ujenzi wa uzio na barabara ili kuupa haiba Uwanja
huo, akibainishaku wa sura ya nchi huanzia pale mtu anaposhuka.
Nae
Katibu Mkuu Wizara Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Amour Hamil
Bakar,alisema ujenzi wa jengo hilo uko hatua za mwisho kukamilika,
ambapo unatarajiwa kukabidhiwa Serikalini mapema mwezi wa Mei, 2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitembelea Jengo jipya la Abiria la Terminal 3 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuangalia maendeleo ya ujenzi huo leo 14-4-2021, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Rahma Kassim Ali na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Ndg.Amour Hamil Bakari, wakati wa ziara yake kutembelea ujenzi wa jengo jipya la Abiria la Terminal 3 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Rahma Kassim Ali na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Dkt.Juma Malik.(Picha na Ikulu).
Alisema,
ujenzi huo umefikia zaidi ya asilimia tisini, na kusema baadhi ya mambo
yatakayoshughulikiwa katika kipindi kifupi kijacho kuwa ni pamoja na
ushughulikiaji wa mifumo ya‘Internet’, mifumo ya Uhamiaji pamoja na
mifumo ya ukaguzi.
Karika ziara hiyo, Rais Dk. Mwinyi alitembelea
maeneo mbali mbali ya jengo hilo, ikiwemo eneo la ukaguzi wa mizigo,
eneo la Usalama , ukaguzi wa Paspoti, eneo la Abiria wanaosubiri ndege,
vyumba vya wageni mashuhuri (VIP), eneo la wasafiri wa nje, eneo la
kupokelea mizigo, eneo la wasafiri wa nje na ndani pamoja na sehemu ya
Abiria wanaosubiri ndege.
Aidha, katika ziara hiyo Dkt. Mwinyi
aliambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwemo Waziri wa
Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Rahma Kassim Ali, Katibu wa Baraza
Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Mkuu wa Mkoa
Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa, pamoja na viongozi wengine wa
Serikali.