Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi sita leo Aprili 21,2021

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi katika vikosi Maalum vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tume ya Uratibu na Udhibiti wa Dawa za kulevya pamoja na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA), anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.
 
Katika uteuzi huo, Rais Dkt. Miwnyi amemteua Kanali Azana Hassan Msingiri kuwa Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Kanali Makame Abdallah Daima kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kanali Rashid Mzee Abdallah kuwa Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Ukozi.

Wengine ni Luteni Kanali Khamis Bakari Khamis kuwa Kamishna wa Vyuo vya Mafunzo, Luteni Kanali Burhani Zubeir Nassoro kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Uratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya pamoja na ACP Ahmed Hamis Makarani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi (ZAECA).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Abdallah uteuzi huo umeanza leo Aprili 21, 2021.

Mnamo Aprili 12, 2021 Rais Dkt. Mwinyi alitengua uteuzi wa Makamanda wa vikosi vitatu vya Idara Maalum za SMZ kufuatia kuwepo kwa wafanyakazi hewa hali iliyosababisha upotevu wa fedha nyingi za Serikali.

Aliowatengua walikuwa ni Kamanda wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Ali Abdallah Ali, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kanali Ali Mtumweni Hamad na Mkuu wa Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) Comodore Hassan Mussa Mzee.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news