Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa
viongozi mbalimbali kama ifuatavyo;
1.
Amemteua
Dkt. Richard J. MASIKA kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia
Dar es Salaam (DIT). Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Aprili,
2021. Dkt. MASIKA anachukua nafasi ya Marehemu Prof. Apollinary Elikana PELEKA.
2. Amemteua Prof. Joseph J. MSAMBICHAKA
kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya
Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC).
Uteuzi huu umeanza tarehe 15
Aprili, 2021. Prof. MSAMBICHAKA anachukua nafasi ya Prof. Manase Peter SALEMA.
3.
Amemteua Dkt. Revocatus Petro MUSHUMBUSI kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI). Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Aprili, 2021. Dkt.
MSHUMBUSI anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ladislaus NSHUBEMUKI ambaye amestaafu.
4.
Amemteua
Prof. John W.A. KONDORO
kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) baada ya kumaliza muda wa kipindi cha kwanza. Uteuzi huu umeanza tarehe
15 Aprili, 2021.
5.
Amemteua
Dkt. Mboni A. RUZEGEA kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba
Tanzania (TLSB). Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Aprili, 2021. Dkt.
RUZEGEA anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na Dkt. Ali MCHARAZO ambaye
amestaafu.
6.
Amemteua Prof. Esther Hellen LUGWISHA
kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kumaliza muda wa kipindi cha
kwanza. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Aprili, 2021.
7.
Amemteua Kept. Ernest Mihayo BUPAMBA
kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Bahari Dar es
Salaam (Dar es Salaam Maritime Institute
– DMI) baada ya kumaliza
kipindi cha kwanza. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Aprili, 2021.
8.
Amememteua Prof. Makenya MABOKO kuendelea
kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) baada ya kumaliza muda wa kipindi cha
kwanza. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Aprili,
2021.
|