Rais Samia asamehe wafungwa 5,001 nchini

Leo Aprili 26,2021 katika kuadhimisha miaka 57 ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 5,001 waliokuwa wakikabiliwa na adhabu ya vifungo mbalimbali, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Wafungwa hao 1,516 wameachiwa huru baada ya kupunguziwa robo ya adhabu zao badala ya punguzo la kawaida la theluthi moja linalotolewa chini ya kifungu cha Sheria ya Magereza sura ya 58 na wafungwa 3,485 wamepunguziwa robo ya adhabu zao badala ya punguzo la kawaida la theluthi moja linalotolewa chini ya kifungu cha 49 (1) cha Sheria ya Magereza sura ya 58.

Aidha,wafungwa 3,485 waliopunguziwa adhabu zao wataendelea kutumikia sehemu ya kifungo iliyobaki.

Rais Samia amewataka wafungwa wote walioachiwa huru kutumia vyema mafunzo waliyoyapata wakiwa gerezani na waungane na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa huku wakiheshimu na kuzingatia sheria.Wakati huo huo Rais Samia amewatakia heri Watanzania wote katika maadhimisho ya miaka 57 ya Muungano na amewataka kutumia siku hii kutafakari juhudi mbalimbali zilizofanyika katika ujenzi wa Taifa na wajibu wa kila mmoja katika kuendelea kujenga Taifa imara.

Rais ameahidi kuendelea kuuenzi, kuulinda na kuundeleza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa manufaa ya Watanzania wa pande zote mbili ambao uliasisiwa siku kama ya leo mwaka 1964.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news